Chapati, vitumbua, sambusa, maandazi kufungwa kwenye magazeti, Maafisa Afya mnamtazamo gani kiafya?

Dom boy

Member
Joined
Jan 24, 2018
Posts
99
Reaction score
64

Katika hali ya mazoea ya muda mrefu, imeshakuwa ni jadi kwa vitafunio hivi wakati wa chai kufungwa ndani ya magazeti unapokwenda kununua kwa baadhi ya watayarishaji, mfano mama lishe.

Nionavyo mimi iko haja ya hao waliodumu katika utamaduni huu wabadike, gazeti toka kiwandani mpaka limfikie muuzaji huwa limeshapita sehemu nyingi, na kwa hali hii sina uhakika na usafi wa gazeti hilo, itapendeza sana kama itabuniwa njia mbadala ya vifungashio hivi.

Je Maafisa Afya wana mtazamo gani juu ya kulinda afya ya mlaji.

Nawasilisha.
 
Nadhani gazeti ni kavu , hivyo halitoi mazingira kwa wadudu kuishi/kukaa kwenye gazeti kwa muda mrefu... Ivyo ndo maana kutoka miaka ya '90 mpaka leo watu wanatumia na hakuna madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…