Chapati zenye nakshi

Chapati zenye nakshi

vanilla

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
448
Reaction score
357
kwa wale wapenzi wa chapati Kama mie Naona mate yashawatoka. Upishi Wa chapati umekua kitendawili kwa warembo wengi sana ila ukishazijulia utakua wazipika kila siku.

Leo naja waletea pishi hili la chapati zenye nakshi za kutosha.

Mahitaji; Unga Wa ngano kilo 1, butter vijiko vinne vya chakula, Maziwa y’a Nido vijiko 10 vya chakula (vijaze), Maji y’a vuguvugu, chumvi, kitunguu saumu, karoti, kitunguu maji, vanilla na Nazi.


Maandalizi;

Anza kwa kusaga punje mbili za kitunguu saumu, kitunguu maji, na karoti moja y’a size, halafu changanya pamoja.

Kwenye chombo cha kukandia tia unga, Nido, chumvi kiasi, halafu weka butter halafu changanya. Baada ya hapo tia ule mchanganyiko wako wa karoti na vitunguu halafu changanya tena.

Baada ya hapo unatia nazi. Kama ni y’a unga basi vijiko viwili vyatosha, ikiwa y’a maji weka robo kikombe halafu anza kukanda. Chukua maji yale ya uvuguvugu tia vanilla kijiko kimoja cha chai halafu anza kuyamiminia kwenye mchanganyiko wako huku ukiendelea kukanda. Hapa maji utakadiria tu kwa kuangalia ulaini Wa unga wako. Endelea kukanda kwa dakika 10 kisha funika uache kwa lisaa limoja.

Baada ya saa moja funua na ukande tena kidogo kisha gawanya madonge madogo madogo. Kwa kilo 2 mimi hutoa chapati 16 hadi 18.

Hapa sasa linafuata zoezi la kupaka mafuta na kukunja. Badala y’a mafuta tutapaka tena butter. Ukishamaliza kupaka mafuta na kukunja zifunike tena kwa dakika 30.

Baada ya dakika 30. Anza kutoa mojamoja, sukuma kisha choma kwa moto mdogo. Katika kuchoma usiweke mafuta pande zote mpaka ziwe zimewiva na rangi y’a kahawia kwa mbaali ili ziive mpaka ndani.

Naamini nimejitahidi kidogo kuelezea pishi hili. Atakaejaribu anaweza kuleta mrejesho.

Enjoy!!!
 
E7EA3B9B-EFD2-4586-A3E8-DE4E492D9EE2.jpeg
57FD3EAC-AAE4-4A6D-9071-E387D255B692.jpeg
60094A17-62A5-4CC4-9057-21FC42A50383.jpeg
 
Back
Top Bottom