Uchaguzi 2020 Charles Kimei unatuaibisha wana Vunjo

Jaman mbona tuna acha asili zetu wakuu
Mila na desturi lazima zifwatwe
Sisi bado ni waafrica
Umagharibi na uarabuu usitufanye kuwa maamuma
Mbona jando tunakwenda au nao uchawi
 
Akifanya Lissu inakuwa sawa, wakifanya Wa Ccm ni uchawi.
 
Kamuua /kamdhuru nani mkuu?
Angekuwa kanisani anafukizwa ubani napo ungesema hivyo?!
Ushirikina si kuua watu. Ushirikina ni kumshirikisha Mungu na hawa miungu wengine. Kimei ni mkristo, anapaswa kuzingatia mafundisho ya kikristo asije akakipatiliza laana kizazi chake au aachane na ukristo azingatie hayo mnayoyaita mila.

Kitabu cha kutoka 20:3-5 Mungu anatuonya tunaomuabudu tusiwe na miungu wengine kwani Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye wivu.
 
tutake radhi. Usi generalise kabila zima. Wengine ni watumishi wa Mungu aliye hai.
Wito kwenu msijaribu kumchanganya Mungu aliye hai na huyo mungu ajulikanaye kama mila na tamaduni.
 
Hizo ni mila na desturi tu kutokana ma kabila husika mi sioni ajabu kabisa.
 
Kushika mila na desturi ni akili.
Lazima ashinde sasa.
 
Mgombea ubunge wa CCM Vunjo, Dr. Charles Kimei anatuaibisha na picha zinazo zunguka kwamba kafanya TAMBIKO ili awe mbunge. Msomi mzima anafanya mambo ya ajabu.

View attachment 1557923View attachment 1557925

Jamani hapo anabarikiwa na wazee wa mila. Je, angekwenda madhabahuni kwa padre au msikitini kwa shehe/imam tungesema hayo?
Katika jambo wazungu walilofanikiwa ni kutufanya tujione "washenzi" na tujichukulie hivyo. Inakuwaje tunajiondoa ufahamu kiasi hicho cha kujidharau na kudharau utamaduni wetu kiasi cha kuufananisha na uchawi? Tujikomboe kifikra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…