Chasambi katukosea heshima wana Simba, atuombe msamaha

Chasambi angesema idol wake ni Ronaldo naamini isingekuwa ishu. Ishu ni kumtaja Max ambaye ni mchezaji wa Yanga.
Sidhani kama issue hapo ni kumtaja Max, halo mkanganyiko umekuja alipokazia kwamba "kwenye timu yangu? Aaaah, hakuna!" Yaani angeenda moja kwa moja kwenye jibu kusingekuwa na sintofahamu hii! Hapo mashabiki wa Makolo wameumia kwa kukandiwa wachezaji wao! Laiti angesema tu, role model wangu ni Max hakuna mtu angejali!
 
Simba haipendi watu wakweli, imejaa wanafiki, wazandiki, mburulaz na mbumbumbu
 
Yuko sawa ,hapo shida ni nini ni kweli huyo ndo anayemvutia kiuchezaji
 
Ni ukweli mtupu.
 
Naunga mkono hoja
 
Fukuza huyo mamluki.
 
Sasa kama hamna, aseme uongo kukuridhisha?
 
Aulizwe tena!, ndio maana wenzao huwa wanaficha Hata midomo ili kuficha maneno yao yasitafsiriwe vibaya.

Dogo yuko sahihi lakini hakuwa makini anapojibu swali la kishari kama hilo.

Ngoja wenzake waache kumpa pasi kama ataweza kukaba na kufunga mwenyewe.

Hata hivyo Max anajituma sana, Simba tumchukue huyu jamaa.
 
Uhuru wa kujieleza uzingatiwe...Mim ni yanga lakini namkubali sana Muhammed Hussein Zimbwe junior...

Maisha sio magumu kiasi hicho mkuu
Kwani yeye angesema anamkubali max kungekuwa na shida gani, kuliko kuweka maneno mengine, huko nyuma aliwahi mtaja Max na hakukuwa na haya maneno
 
Acheni ushamba na upumbavu nyinyi. Huyo Maxi Nzengeli alipohojiwa mchezaji gani anayempenda akamtaja Awesu Awesu wa Simba, mbona wanayanga hawakumshambulia?.

Hizi ni timu za mpira sio dhehebu la dini, punguzeni mawazo ya kijinga.
 
Kwani yeye angesema anamkubali max kungekuwa na shida gani, kuliko kuweka maneno mengine, huko nyuma aliwahi mtaja Max na hakukuwa na haya maneno
Kikosi cha kwanza cha Lionel Messi kina Cristiano Ronaldo ndani yake, hayo ni mawazo binafsi ya mchezaji mwenyewe na hakuna mwenye haki ya kumpangia wala kumuingilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…