Chatanda afurahishwa na Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilayani Chato

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amefurahishwa na Utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani Chato Mkoani Geita alipotembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika wilaya hiyo .​

Akizungumza leo katika Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato Mwenyekiti Chatanda amewapongeza viongozi wa Serikali chini ya Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedith Katwale ambaye ameshirikia na Mkurugenzi wake wa Halmashauri kwa usimamizi na Ufanisi wa hali ya Juu .

" Fedha ya Serikali zaidi ya Bilion 31 imejenga Hospitali hii ya Kanda ya Chato niwaombe wauguzi wa Hospitali hii muwahudumie wagonjwa vinzuri kwa kuwa wananchi mbalimbali watakuja kutibiwa hapa hivyo Uadilifu, upendo na hekima ili wananchi wafurahie matunda ya Rais Samia kwa upande wa afya katika kupata huduma bora kwa wauguzi wao."

MWISHO.

 
Natarajia Stephano Mgendanyi na ChoiceVariable nyie wote mnatoka chama cha kijani (CCM) au serikali iliyopo madarakani kwa sasa. Lakini taarifa zenu zina iinzana sana sijui ni kwa lengo la kuandaa mkkati fulani kwa faida ya mmojawapo sijui.
Stephano Mgendanyi umetuonesha tena kwa picha kwamba utekelezaji wa ilani ya CCM wilayani Chato imefanikiwa lakini mwenzio Choicevariable ametoa taarifa za kuunga mkono kwamba Kalemani hatakiwi na wananchi wa Chato kwamba hakuna chochote alichokifanya zaidi ya jitihada binafsi za JPM hapa tuwaeleweje?

Kumbukeni JPM hakubaugua ndio maana pamoja na kwamba ni mfu lakini bado mawazo ya wananchi wanasema ndio walimpenda sana kulinga viongozi wengine wa kitaifa na kura hii ya kimtandao inathibitisha hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…