Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
CHATANDA: "IGUNGA MMEPATA MBUNGE MCHAPA KAZI"
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda Amempongeza Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa kwa nidhamu yake ya uchapakazi na uwajibikaji kwa Wananchi wa Jimbo la Igunga.
Mhe.Chatanda (MCC) Amesema hayo akiwa Ofisi za CCM Wilaya ya Igunga ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara ya Kikazi kwenye Mkoa wa Tabora;
"... Jimbo la Igunga Mmebahatika kupata Mbunge mchapakazi na mwenye nidhamu ya kujituma mpeni ushirikiano. Nimekuwa Nikimfuatilia kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali Ninaona taarifa zake akichapa kazi bila kuchoka. Huyu kijana Ninampenda sana ila kwa uchapakazi kazi wake na nidhamu ya kujituma kuwatumikia Wananchi..."
Mhe. Chatanda (MCC) Ameambatana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC) na Wajumbe wa Kamati ya Utekekelezaji wa UWT Taifa Mhe. Hawa Ghasia na Mhe. Subira Mgalu.