ChatGPT sasa kuchukua nafasi za consultants/ Therapist

matemabi

Senior Member
Joined
May 2, 2017
Posts
113
Reaction score
145
Leo nimeamka katika pita pita zangu za kusoma na kupata vitu vipya katika maswala ya akili mmnemba nikagundua kwamba kupitia ChatGPT sasa unaweza kuongea nayo na ikakujibu kila aina ya swala utakalo uliza na kwa sasa ni bure kabisaaa... ambayo zamani ulitakiwa kulipia ambapo baadhi yetu ilikuwa inatukatisha tamaa hivi mana tunape da mleleko...

Sasa mseleleko umetufikia...

Ipo hivi, kwa kuongea na chatGPT unaweza kuifanya kuwa business consultant, financial, relationships au mambo mengine. Imagine kama utakuwa na haja ya kwenda kwa watu wenye biashara hizo na wakati wewe unaweza kuuliza kwenye akili mnemba hapo hapo na ukapata jibu right away.

Unaweza kuuliza maswali zaidi na kufanya reasoning ya kutosha kupata logic and guidance on what to do.


Anyways dunia ina evolve sana...

Sent from my SM-N976N using JamiiForums mobile app
 
Hyo kitu kiboko yani binafsi hata matumizi ya google nimepunguza. Hio ngoma ni shida unaweza andaa point zako au analysis zako za mambo unayotaka kujua na ikakupa kila kitu.

Imekua kama ubongo wa ziada kitu hujui au huelewi unai command inakusaidia kung’amua mambo / hard / complicated topics alaf inapiga mule mule very accurate.

Hii ita badilisha sana namna ya usomaji kwa wanafunzi vyuoni na shuleni. Ngoma inakutolea hadi notes / material wewe tu ujue unataka nini.
 
Akili za bangi izi mkuu!
AI has no ability to perceive human feelings, itakupa majibu on the basis of logic haiwezi kuzingatia emotions.
Kwa upande wa Therapy, huenda huelewi How things work, Kwenye kucope na emotions binadam sio tu tunahitaji kueleza mtu then based on the logic aanze kushuka kukueleza maparagraphs HELL NO ! but we need to feel connected to that person, (Sisi engineers tunaita Synchronization, wabobezi wa Civics wanaita Empathy) and only through that a victim can feel at ease.
 
Bado binadamu ana umuhimu hapo
 
Kulikuwa hakuna haja ya kusema neno bangi... ila umeongea kiustadi sana.

Kila mtu ana hitaji lake kwa kipimo chake, mimi naona inafaa, kama kwako haifai basi sawa mkuu!

Sent from my SM-N976N using JamiiForums mobile app
 
Mimi natumia Gemini ya google iko vizuri sana pia. Sauti wameiboresha inakuwa kama ya binadamu kabisa unasikia hata anavyovuta pumzi.

Hii unapiga nayo stori simu umeiweka pembeni kidogo hapo raha yake utumie kingereza inaelewa haraka.
 
Inaenda kutengeneza kizazi cha hovyo kwani vijana wengi watashindwa kufanya utafiti kwa kutegemea akili zao badala yake wakitegemea chtgpt .
Ninao vijana waliomaliza chuo wapo kama intern kazini kila unaemuuliza andai chartgpt ilimsaidia sana kwenye project.
Hata mimi mwenyewe naitumia kwenye kuandika report pia ha haha .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…