Chato Airport ni kaa la moto lisilozimika kwa CCM na Magufuli. Sasa anaahidi kujenga Airport kama ya Chato kila anakopita...!

Chato Airport ni kaa la moto lisilozimika kwa CCM na Magufuli. Sasa anaahidi kujenga Airport kama ya Chato kila anakopita...!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Sasa hali si hali kambi ya mgombea Urais - CCM Mzee Pombe Magufuli.

Chato Airport ya kijijini na shambani kwake inamtesa yeye, inawatesa CCM wote maana haina utetezi wenye macho na akili watu wakaelewa.

Sasa kama kujifariji na kujidanganya, kila mahali anapopita anamwaga ahadi za kujenga Chato Airports kote kote.

Katoa ahadi ya kuwajengea Chato International Airport wana Njombe....!!

Katoa ahadi ya kuwajengea CHATO AIRPORT wana Kigoma...!!

Katoa ahadi ya kuwajengea nao CHATO AIRPORT wana Bukoba, Karangwe na kotekote anakopita....!!

Leo tena ahadi ni za kujenga CHATO AIRPORT ni za kumwaga kila mji na kijiji atakachopita.

Ukistaajabu ya Mussa, basi subiri uyaone ya Firauni. Huyu ndiye Magufuli bwana, msukuma jeuri asiyejali chochote....!!

Chato Airport kweli ni kaa la moto, halizimiki hata kuleta kikosi cha Zimamoto cha Ukonga...

Kuzimika kwake, ni mtu kufukuzwa atoke kwenye ofisi za umma, baaaaasi....
 
Kafanya mengi mazuri kwenye miuondo mbinu na mawasiliano. Ila ili la CHATO International airport CCM wasiliongelee kwenye kampeni zao linaleta maswali ambayo hayana majibu
 
Kha!!, kwani nini cha ajabu sasa,kwani Chato ipo Burundi ama Rwanda?
 
Msaada unakata ndani ya chama, baadhi watainuka wakiwa wao kimwili ila kiroho ni watu tofauti...
 
Kafanya mengi mazuri kwenye miuondo mbinu na mawasiliano. Ila ili la CHATO International airport CCM wasiliongelee kwenye kampeni zao linaleta maswali ambayo hayana majibu
umebadirika yaani ulivyo CCM leo naona uko pole pole kuelekea Kwa Lisu hongera
 
Kwanini iwe kelele kwa Chato iliyopo Geita mkoa wa kilimo na dhahabu?
Walau mngepeleka Geita mjini au kahama!Lakini mnaoeleka uwanja kijijini kisa tu kazaliwa Rais huko!!!Sio sawa!
Tokea uwanja ukamilike,abiria pekee waliotua hapo ni Magufuli,Uhuru na Museveni!
Kikwete angekuwa na akili kama za Magu,Msoga kungekuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa!
 
Upinzani ulisha kufa tangu 2015, kilichobaki ni futuhi.
 
Kinacho muuma ata hao wana chato wame mgeuka bado haamini

SUBIRI KIDOGO
 
Back
Top Bottom