Chato: Raia wa Burundi akamatwa na AK47 iliyotumika kwenye mauji ya mchimbaji madini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema wanamshikilia raia huyo kwa tuhuma za kuingia Nchini kinyume cha Sheria na kumiliki silaha ambayo imekuwa ikitumika katika matukio ya uhalifu

Kamanda amesema silaha hiyo ilitumika kwenye mauaji ya mchimbaji mdogo Tegemeo Rashid aliyeuwawa Novemba 2, 2022 katika Kata ya Buziku wilayani Chato

Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa wanne waliohusishwa na mauaji hayo ambao wamekiri makosa na kumtaja mmiliki wa AK47 kuwa ni raia wa Burundi.

====================

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamushikilia raia wa Burundi kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria pamoja na kumiliki silaha aina ya AK47 ambayo imekuwa ikitumika katika matukio ya uharifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari na kueleza raia huyo ametiwa mbaroni baada ya silaha hiyo kutumika kwenye mauaji ya mchimbaji mdogo Tegemeo Rashid (38) Novemba 2, 2022. Rashidi aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye makali shingoni na kichwani kijijini Ihanga, Kata ya Buziku wilayani Chato.

“Wakati wa utekelezaji wa mauaji hayo, wauaji walikuwa na silaha aina ya AK47 ambayo waliitumia kumutishia marehemu asimame wakati akiendesha pikipiki na ndipo walifanikiwa kumkamata.

“Kisha walimufunga kwa kamba ya katani shingoni na kumzungushia tumboni na mikononi na kumbuluza hadi umbali wa mita 170 toka eneo walipomusimamisha na kufanikisha adhima yao. “Wakati wa kutekeleza mauaji hayo, alijitokeza msamalia mwema akitaka kumuokoa marehemu ndipo majambazi hao kwa kutumia silaha hiyo walifyatua risasi hewani ili kumtisha ashindwe kutoa msaada.”

Amesema jeshi la polisi limefuatilia na kufanikiwa kuwakamata watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo ambao wamekiri kuhusika na kisha kumtaja mmiliki wa AK47 kuwa ni raia wa Burundi.

“Juhudi zilifanyika na hatimaye jana usiku (Novemba 4) tulifanikiwa kumkamata huyo mrundi, lakini katika mahojiano aliweza kutuonyesha silaha aina ya AK47, ambayo haina namba za usajili ikiwa na risasi 11.

“Lakini pia amekiri kwamba anatokea Burundi na wenyeji wake ni watuhumiwa ambao walimpokea hapa kwetu kutuonyesha Bunduki hiyo ambayo alikuwa ameificha kwenye shamba la mahindi katika kijiji cha Buziku.” Ameeleza Kamanda.

Kamanda Jongo amesema jeshi la polisi linaendelea kukamilisha hatua za kisheria ili kuwafikisha mahakmani watuhumiwa hao.

HABARI LEO
 
Awamu ya jamaa haya yalidhibitiwa, ila huu ndio muda wao!! Kila mwanadamu ana mazuri yake na upande wapili.
 
Sasa mpaka asiye raia anaingia interior ya nchi umbali kadhaa kutoka mpakani akiwa amebeba silaha ya kivita anaishia na kujimudu akitenda yampendezayo, je ndugu polisi mlikuwa wapi? Ndugu uhamiaji mlikuwa wapi? Kuamini polisi wa nchi hii unatakiwa kuwa na akili za kiwendawazimu wazimu hivi!
 
Awamu y mwenda zake yalikua yanafichwa matukio kama haya
Kwa sababu ya sera yake ya: "kukamata haraka haraka" au kwa msemo mwingine ni jio kwa jino.

Nadhani dawa ya ujambazi ni hiyo, maana kwenye vyombo vya sheria wana mtandao mkubwa pamoja na rushwa iliyotamalaki.
 
M23 baada ya kuona congo kugumu wanakuja TZ sasa
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema wanamshikilia raia huyo kwa tuhuma za kuingia Nchini kinyume cha Sheria na kumiliki silaha ambayo imekuwa ikitumika katika matukio ya uhalifu

Kamanda amesema silaha hiyo ilitumika kwenye mauaji ya mchimbaji mdogo Tegemeo Rashid aliyeuwawa Novemba 2, 2022 katika Kata ya Buziku wilayani Chato

Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa wanne waliohusishwa na mauaji hayo ambao wamekiri makosa na kumtaja mmiliki wa AK47 kuwa ni raia wa Burundi.

====================

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamushikilia raia wa Burundi kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria pamoja na kumiliki silaha aina ya AK47 ambayo imekuwa ikitumika katika matukio ya uharifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari na kueleza raia huyo ametiwa mbaroni baada ya silaha hiyo kutumika kwenye mauaji ya mchimbaji mdogo Tegemeo Rashid (38) Novemba 2, 2022. Rashidi aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye makali shingoni na kichwani kijijini Ihanga, Kata ya Buziku wilayani Chato.

“Wakati wa utekelezaji wa mauaji hayo, wauaji walikuwa na silaha aina ya AK47 ambayo waliitumia kumutishia marehemu asimame wakati akiendesha pikipiki na ndipo walifanikiwa kumkamata.

“Kisha walimufunga kwa kamba ya katani shingoni na kumzungushia tumboni na mikononi na kumbuluza hadi umbali wa mita 170 toka eneo walipomusimamisha na kufanikisha adhima yao. “Wakati wa kutekeleza mauaji hayo, alijitokeza msamalia mwema akitaka kumuokoa marehemu ndipo majambazi hao kwa kutumia silaha hiyo walifyatua risasi hewani ili kumtisha ashindwe kutoa msaada.”

Amesema jeshi la polisi limefuatilia na kufanikiwa kuwakamata watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo ambao wamekiri kuhusika na kisha kumtaja mmiliki wa AK47 kuwa ni raia wa Burundi.

“Juhudi zilifanyika na hatimaye jana usiku (Novemba 4) tulifanikiwa kumkamata huyo mrundi, lakini katika mahojiano aliweza kutuonyesha silaha aina ya AK47, ambayo haina namba za usajili ikiwa na risasi 11.

“Lakini pia amekiri kwamba anatokea Burundi na wenyeji wake ni watuhumiwa ambao walimpokea hapa kwetu kutuonyesha Bunduki hiyo ambayo alikuwa ameificha kwenye shamba la mahindi katika kijiji cha Buziku.” Ameeleza Kamanda.

Kamanda Jongo amesema jeshi la polisi linaendelea kukamilisha hatua za kisheria ili kuwafikisha mahakmani watuhumiwa hao.

HABARI LEO
Hata waliohukumiwa Dar es Salaam kwa mauaji ya Mzungu Loter pia Hit Man alikuwa Mrundi.
 
Back
Top Bottom