Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
WAUGUZI wawili wa Kituo cha Afya cha Bwanga wilayani Chato mkoa wa Geita, wamehamishwa, kwa kutuhumiwa kuomba Sh. 90,000 kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa.
Wanadaiwa kuomba fedha hizo kwa wagonjwa ili kuitumia kama nauli kwenda kufuata damu katika vituo vingine vya afya kutokana na kituo kukosa huduma ya damu.
Wauguzi wanaotuhumiwa ni George Makoye na Godfrey Willison, ambao wanadaiwa kuchukua fedha hizo kwa ndugu wa wagonjwa.
Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, Leonidas Felix, alisema baada ya kufanya uchunguzi walibaini kuwatoza wagonjwa Sh. 90,000 kama nauli waliyotumia kwenda kutafuta damu kwenye kituo kingine cha afya.
“Kufanya hivyo walikiuka kanuni na taratibu za utumishi wa umma, kwa sababu hata uongozi wa kituo hicho haukupewa taarifa,” alieleza Felix.
Alisema wauguzi hao wamerejesha fedha hizo kwa wagonjwa.
“Tayari wauguzi hao wamelipa faini na hawatashitakiwa tena kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuwapa adhabu mara mbili,”alisema Felix.
“TAKUKURU tunaitaka mamlaka ya nidhamu iwahamishe wauguzi hao na iwapeleke katika vituo ambavyo havihusiki na damu salama,” alisema Felix.
“Watu wakibainika na makosa, huwa tuna mambo mawili; kuwapeleka mahakamani au kuwachukulia hatua za nidhamu, lengo ni kutoa fundisho kwao na kwa watumishi wengine wenye tabia kama zao.”
Felix, alisema wauguzi hao kwa sasa wameshamishiwa katika vituo vingine, ambavyo havina huduma ya damu salama.
NIPASHE