Mwenyekiti wa Makatibu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Basil Lema amesema wamekuwa wakifanya siasa kwa ugumu katika chama hicho kwani wamekuwa wakionekana kama kivuli cha Chama cha Mapinduzi(CCM) kutokana na mienendo iliyokuwepo.
Lema amesema hayo leo Julai 13, 2026 akieleza kuwa sasa wamechoka na wameamua kufanya siasa za kweli na hawapo tayari kuonekana kwa taswira hiyo.
"Tumefanya siasa ambapo tulikuwa tukitafsiriwa kwamba sisi ni CCM B kwa muda mrefu. Tukipita mitaani watu wakituangalia wanatuogopa wasaliti hao, tunafanya siasa watu wanajua kabisa sisi ni waigizaji ingali mioyo yetu ina hasira inayotaka kubadili nchi. Sasa tumeamua kwa bei yoyote ile anayetoboa mtumbwi atupishe ili safari iendelee ametupisha nyinyi mnaturudisha kwa ajii ya chakula cha tumbo lenu hatutakubali" amesema Lema
Ha ha ha.. too late. π
Akina Mrema waliwezaje kum "outsmart" mtu kama Hashimu Rungwe!
Msomi kabisa akashindwa ng'amua hii project ya hela.. π
Bongo mimi siji kuhama wazee! π
Tunakazi nzito ya kuijenga chauma,hasa nguvu kubwa iwekwe matawini na kwenye mashina!..na huu ndiyo msingi mkuu wa chama kinachotaka kuwa imara!..tuwafunze vijana uzalendo halisi,tuepuke wanachama bendera fuata upepo kama wale wa chadema!...