Chawa mwanadamizi Mwijaku atoa povu baada ya TRA kumtaka alipe kodi

Chawa mwanadamizi Mwijaku atoa povu baada ya TRA kumtaka alipe kodi

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Nikajua ukiwa chawa, haubugudhiwi.🤣🤣

TRA wamefatilia makampuni ambayo Mwijaku anayotangaza biashara nao, na kutaka makampuni hayo yalipe kodi kwa mamlaka hiyo.

Mwijaku baada ya kupata taarifa hiyo akatoa povu. Hajaamini macho yake.

TRA nyoosheni hivyohivyo, hakuna kucheka na wowote
IMG_5413.jpeg
 
Eti kama love kwao, kwahiyo nawale wanaofanya kazi nao wasilipe Kodi wawe wanasema wanajitolea tu pia.

TRA hawa wasanini muanze kuwakaba sasa kwenye Kodi maana wanatuambia sanaa inalipa sana na kupitia sanaa wanatuonyesha maburungutu ya hela mitandaoni.

Sanaa ni kazi kama kazi nyingine, Kila msanii awe wa leseni na akadiliwe mapato yake akatwe Kodi kama wafanyabiashara wengine., msisubiri msanii afungue duka ndio muanze kumdai Kodi.

Doto Magari ni influence awe na leseni ya kazi anavyofanya, alipe Kodi, madalali wa magari wawe na leseni na Kila dili wanayofanya walipwe Kodi nao.

Nimewasaidia kuwaonyesha vyanzo vya mapato mkalipe Kodi sasa.
 
Tusitegeane kulipa kodi TRA wekeni utaratibu mzuri wa kukusanya kodi kwa madalali,wasanii,wabunifu.
Kulipa kodi ni wajibu sio adhabu.

Pamoja tunajenga taifa Letu
 
Mwijaku lipa Kodi kwa matangazo unayofanya acha ushamba wewe ,kulipa Kodi ni sifa ya uzalendo. Wewe na wenzako machawa kina dotto magari,baba levo,lipeni Kodi sio mnajisifia mna Hela halafu Kodi hamlipi.TRA Daini Kodi kwa wafuatao, comedian wote,ma mc wote,wapambaji wa maharusi,wapisho ktk harusi,misiba,sherehe, wanamziki wa bongo flava,wachambuzi wa soka ktk blogs zote
 
Hivi hizo kampuni wanazozitangaza zinashugulika na nini???

Ova
 
Dotto naye think tank yao 😄

Ova
 
Nikajua ukiwa chawa, haubugudhiwi.🤣🤣

TRA wamefatilia makampuni ambayo Mwijaku anayotangaza biashara nao, na kutaka makampuni hayo yalipe kodi kwa mamlaka hiyo.

Mwijaku baada ya kupata taarifa hiyo akatoa povu. Hajaamini macho yake.

TRA nyoosheni hivyohivyo, hakuna kucheka na wowoteView attachment 3247954
Sheria ifuatwe, Mwijaku alipe kodi
 
Tusitegeane kulipa kodi TRA wekeni utaratibu mzuri wa kukusanya kodi kwa madalali,wasanii,wabunifu.
Kulipa kodi ni wajibu sio adhabu.

Pamoja tunajenga taifa Letu

kabisa. Hawa ndio wanashabikia wengine wakiangushiwa majumba yaliyochakaa sababu wana amini wako karibu na watoa maamuzi
 
Wamfate yeye kama nani. TRA kazieni hapo hapo
 
Back
Top Bottom