Chawa wa CCM wanalitambua hili?

Chawa wa CCM wanalitambua hili?

iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,039
Reaction score
4,889
Hili suala la ushoga na LGBT kwa ujumla limekaa vibaya kwa siasa za kimataifa. Binafsi nadhani ni kitu ambacho itabidi kutoongelea kabisa au kuongelea kwa tahadhari kubwa.

Ni kweli kama nchi ina watu wengi ambao hatupendi hili jambo, lakini pia tukumbuke hatuko peke yetu duniani. Ndo maana hata Serikali hawawezi kuliongelea na kutoa mwelekeo kwamba sisi kuhusu LGBT mwelekeo wetu ni huu.

Sasa imezuka tabia ya Chawa wengi wa CCM huko mitandaoni sasa hivi kujaribu kuhusisha chama cha CHADEMA kuwa kina support ushoga. Unapo unaposema CHADEMA wana support Ushoga maana yake unasema CCM hawa support ushoga.

Hivi wanajua madhara ambayo tunaweza kupata kama nchi kwa ujinga huo wanaofanya?

Je, wanajua kwamba kwa kuihusisha CHADEMA na ushoga wanaipalia moto CCM?

Nadhani pamoja na uchawa inabidi tuweke maslahi ya nchi mbele. Chawa wa vyama vyote wanatakiwa kujua ni nini cha kuongea na kipi si cha kuongea hasa linapikuja suala la mahusiani ya kimataifa.

Ni hayo tu
 
Saivi wanapigana wao kwa wao ikifika karibu na uchaguzi wanayupigania sisi kwa khanga na kofia baada ya hapo mpaka 2030 tena.... Mimi sina chama Mungu akishanibariki mahitaji yangu kwisha sitaki kingine
 
Mie nilivyosikia ile kauli ya papa nikaja shetani amecheza karata zake amelitwaa kanisa bado tu waumini kuanza kugongana maana ni rukhsa sasa
 
Back
Top Bottom