Abtali mwerevu
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 665
- 515
Na: Mwalimu Makoba
Tazama nikamuita mwanangu mpendwa, naye nikamtuma aende mjini akalete vitumbua ili tupate kushtua matumbo. Nilimwelekeza aende kwa Mama Abdul, mama muungwana, mtenda haki na kamwe hakupunja katika kipimo chake.
Nami nikapanda juu ya mlima ili niweze kujionea yanayoendelea. Nikamuona Mama Abdul akipika vitumbua, pembeni kazungukwa na chawa, mbele kidogo kuna wateja waliohitaji kununua vitumbua hivyo! Wateja wapo kimya wanasubiri vitumbua, chawa wanamsifia kwa mapishi yake. Naye awekapo vitumbua vilivyoiva katika sufuria, chawa wanachukua na kula, wengine walimeza bila kutafuna huku wakimwagia sifa lukuki.
Nikaliona kundi la pili lililohitaji kununua likiwa limechoka kusubiria, taratibu wakaanza kuondoka mmojammoja, wengine waliondoka wawiliwawili. Waliondoka taratibu mpaka walipoisha wote! Wakabaki chawa, wanakula vitumbua bila kushiba. Mwanangu mpendwa alikuwa wa mwisho kuondoka, aliondoka na pesa yake mkononi tena akiimba, “Baba kanituma vitumbua tisa na chenji nirudishiwe!”
Tazama ikafika jioni mwangaza ukapotea, sikuweza kuyaona yaliyoendelea, nami nikatamani sana kuyaona lakini sikuweza tena. Niliambulia kusikia makelele ya chawa wakishangilia, “vitumbua vitamu! Hiki cha sasa kiboko… unga umekaa mahali pake, sukari imekadiliwa, moto kidogo mafuta kiasi na laini kutafuna… vitumbua hoyeeeee!”
Wakati nashuka mlimani nikawaza, kama vitumbua vyote vimeliwa na chawa, na hakuna senti moja aliyoingiza Mama Abdul ni wapi atapata fedha ya kununulia unga ili apike vitumbua vingine hiyo kesho?
Nami nikiisha kushuka mlimani, nikabaini kuwa, wafanyabiashara wana siri nyingi!