Chawa wanapokuwa washauri wa viongozi wetu

Chawa wanapokuwa washauri wa viongozi wetu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Tatizo la nchi yetu lipo kwenye vyombo vya habari na mahakama.

Mahakama ikikutana na CCM inakuwa mbendembende. Vyombo vya habari vikiiona CCM vinapatwa na mchecheto..

Matokeo yake nchi sasa washauri wakuu wa viongozi wetu ni watu wa hovyo hovyo wanaoitwa "chawa"

Na bahati mbaya sana hao chawa mpaka watu wazima na wasomi nao wamekuwa chawa.

Lakini imekuwaje watu wa maana wameacha kuwa washauri wa viongozi wetu badala yake chawa ndiyo wameshika usukani!!?
 
Tatizo la nchi yetu lipo kwenye vyombo vya habari na mahakama.

Mahakama ikikutana na CCM inakuwa mbendembende. Vyombo vya habari vikiiona CCM vinapatwa na mchecheto...
Njaa imehamia Kichwani

Na wanafikiri kwa kutumia matumbo 🙄😳
 
CCM ndio tumaini la watanzania na chama kilicho beba Matumaini ya kila mtu mwenye ndoto katika Taifa letu. Ni chama ambacho kinamhakikishia mtanzania kesho iliyo bora kuliko leo , jana na juzi. Ndio maana kinaaminika ,kukubalika na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania wenye akili Timamu na wanaojitambua.zingatia maneno wenye akili Timamu na wanaojitambua.
 
Kwa hapa tulipo yatupasa tufanye mawili
i) Tuwe chawa wote
ii) Tukinukishe kama majirani zetu
Ha ha ha ha

Mzee, kwa Taifa hili option ni moja tu - wote tuwe machawa ili tupate mkate wetu wa kila siku kutoka kwa watawala kutokana na urefu wa kamba ya kila mtu.

Hamna namna nyingime mzee wangu, uzezeta ni mkubwa usio na mfano.
 
Mwijaku ameomba Kozi ya Uchawa itolewe pale Chuo Cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama 😃
 
Mwijaku ameomba Kozi ya Uchawa itolewe pale Chuo Cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama 😃
Haya ndiyo ma vijana ya hovyo kabisa katika nchi. Mwalimu alilijenga Taifa hili ili liwe chimbuko la kuhoji why & how.. hasa kwa vijana.
Mijitukama hii ni ya kutebgwa na jamii na haitufai kabisa.
 
Ha ha ha ha

Mzee, kwa Taifa hili option ni moja tu - wote tuwe machawa ili tupate mkate wetu wa kila siku kutoka kwa watawala.

Hamna namna nyingime mzee wangu, uzezeta ni mkubwa usio na

Ha ha ha ha

Mzee, kwa Taifa hili option ni moja tu - wote tuwe machawa ili tupate mkate wetu wa kila siku kutoka kwa watawala.

Hamna namna nyingime mzee wangu, uzezeta ni mkubwa usio na mfano.
Tukichaguwa kuwa chawa wote, watawala watashindwa wampe nani wamwache nani, hapo sasa ndo hata machawa wataona uchawa siyo dili tena, wataamua kusimamia ukweli
 
Tukichaguwa kuwa chawa wote, watawala watashindwa wampe nani wamwache nani, hapo sasa ndo hata machawa wataona uchawa siyo dili tena, wataamua kusimamia ukweli
Ha ha ha

Mkuu chawa hashindwi pa kukugada, akikosa kwenye ukosi wa shati basi atavamia kwenye upindo wa nguo ya ndani..napo akiona hapafa basi chini ya maskio.
Chawa ni mtu mshenzi sana.

Taifa la ku support uchawa ni Taifa lililokufa.
 
Tatizo la nchi yetu lipo kwenye vyombo vya habari na mahakama.

Mahakama ikikutana na CCM inakuwa mbendembende. Vyombo vya habari vikiiona CCM vinapatwa na mchecheto...
Kwa sababu uwezo kwa kufikiri na kuchanganua mambo kwa viongozi wetu umekuwa mdogo mno, wenye upeo mpana wameamua kukaa pembeni hata kama wengine wapo serikalini ili waone kitakacho tokea.
 
Kwa sababu Viongozi wameilea mno Tabia ya kusifiana.Wanafurahia mno kusifiwa kuliko kukosolewa.

Mazoea zamezaa tabia tayari,hatuna cha kufanya tena.
 
Chawa
Tatizo la nchi yetu lipo kwenye vyombo vya habari na mahakama.

Mahakama ikikutana na CCM inakuwa mbendembende. Vyombo vya habari vikiiona CCM vinapatwa na mchecheto..

Matokeo yake nchi sasa washauri wakuu wa viongozi wetu ni watu wa hovyo hovyo wanaoitwa "chawa"

Na bahati mbaya sana hao chawa mpaka watu wazima na wasomi nao wamekuwa chawa.

Lakini imekuwaje watu wa maana wameacha kuwa washauri wa viongozi wetu badala yake chawa ndiyo wameshika usukani!!?
kama viumbe hai wanakaa kwenye uchafu.

Hapana shaka hawa chawa-waru nao ni hivyo hivyo wakitofautiana na wenzao tu kwenye aina za uchafu.

Ila dawa ya vermins(chawa, kunguni, kupe n k ni kuwa exterminate tu.
 
Back
Top Bottom