LGE2024 CHDEMA: Mkoa wa DSM wenye Mitaa 636 Wamekatwa majina ya Wagombea wetu 571 wamebaki 45 tu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
ASKOFU ATATIZWA SABABU ZA KUTEULIWA WAGOMBEA WA CCM NA KUENGULIWA KWA WAGOMBEA WA CHADEMA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Ndugu Watanzania!
Tumeletewa malalamiko yafuatayo kuhusu uteuzi wa majina ya Wagombea wa Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika Mtaa wa Stop Over (Kimara), Kata ya Saranga katika Manisapaa ya Ubungo yaliyobandikwa muda mfupi uliopita:

1. Alex Fabian Msuka aliomba kuwa Mgombea kupitia CCM na ameteuliwa kuwa Mgombea. Kwa mujibu wa Fomu yake, aliandika kuwa ni MFANYABIASHARA.

2. Godfrey Benedictor Missana aliomba kuwa Mgombea kupitia CHADEMA lakini hajateuliwa. Kwa mujibu wa Fomu yake, aliandika kuwa ni MJASILIAMALI

Sababu iliyotolewa ya kutokuteuliwa kwake ni kuwa ndugu Missana hajaainisha shughuli maalum anazozifanya kutokana na Kanuni ya 15 (D). Ushahidi wa hayo umeainishwa katika fomu za wahusika, Missana na Msuka.

Je, kuna tofauti gani kati ya mfanyabiashara na mjasiliamali? Je, mtu kuandika mfanyabiashara bila ya kuainisha aina ya biashara anayofanya; na mtu kuandika mjasiliamali bila ya kuainisha aina ya ujasiliamali anaoufanya kuna tofauti?

Je, unafikiri ya kuwa Missana wa CHADEMA ameenguliwa kihalali na Msuka wa CCM ameteuliwa kihalali? Je, unafikiri kuwa haya ni mazingira yanayoashiria Uchaguzi huru na wa haki? Je, kama katika mambo yaliyo wazi kama hili yanazua tafsiri tata na kutokea kutokutenda haki, inakuwaje katika zoezi la kuhesabu kura ambalo litakugubikwa na usiri mkubwa?

Kufuatia hili, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa mamlaka ya juu kuangazia suala hili la Mtaa wa Stop Over. Kama ikionekana kuwa Missana ameenguliwa kwa hila arudishwe na hao waliomuengua waondolewe katika zoezi la kusimamia Uchaguzi huu katika Mtaa wa Stop Over. Na kuwa hii ifanyike pia mahali pengine kote ambako itaonekana hujuma kama hii pia imefanywa kwa makusudi.

Sisi ni sauti ya dhamiri katika Uchaguzi huu na hivyo tunao wajibu tuliopewa na dhamiri kuu ili kihakikisha kuwa sauti ya haki haikauki katika taifa letu na dhamiri iliyo kuu hainyauki kabisa!
Je, kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 8 Novemba 2024; saa 8:00 alasiri
 
CCM ni wapumbavu sn
 
Tatizo ni kucheka na nyani lazima akuachie mabua
 
Wengi hawajui kusoma na kuandika, ilibidi Meya mstaafu awatafutie watu wa kuwajazia fomu
HAmna kitu kama hiko,Chadema walitoa wito kwa wagombea wao wote wawe angalau wana elimu ya form six,sasa hawo ambao hawajuwi kusoma na kuandika wametoka wapi tena? Nna imani Chadema kila kanda wakiweza kufuatilia huu uchaguzi kwa karibu wanaweza kulishangaza Taifa,maana raia mtaani wanatamani Chadema itawale ila tatizo ni ukataji wa wagombea,wizi wa kura,na hakuna hatua zozote za makusudi zinazochukuliwa kukomesha hali hiyo.
 
CHADEMA vs serikali/dola

Wananchi = watazamaji

Nani hasa wa kuombewa? CHADEMA au Watanzania?
 
Huyu ni mzuaji wa visa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…