bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Yes Che mallone beki kutoka Cameroon aliyesajiliwa kwa mikwara mingi kutoka Cotton sports ya kwao Cameroon ulikua ni muda tu hujafika kuona panapovuja waswahili wanasema wacha inyeshe tuone panapovuja.
Jumapili Yanga ilikua mvua kubwa na ilinyesha haswa tukaona pale Simba panapovuja kama ni matundu yanayopitisha mvua pale Simba ni Mengi mnoo palivuja haswa sio yule kiungo wao aliyeibwa airport wala mzee wa kuchapa Inonga wala beki wa Yeriko Che malone au mshambuliaji wa Etoo Onana.
sio Ajabu leo wanasimba wote tunataka kikosi kivunjwe chote na tuanze upya au kuwapandisha hata madogo wa under 20 waje wacheze, zile sifa zote za Wachambuzi leo wanasimba hawataki kuzisikia kabisa washafahamu walikua wanapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
Back to the topic Che Malone kwa sisi tunaoutazama mpira kwa jicho la tatu bado hana vigezo vya kuitwa beki katili ni mzito hana kasi kwa kifupi anacheza soft football sema tu ligi yetu inakosa washambuliaji wakali kwangu bado Onyango mtu chuma anakua beki bora kwanza ana mbio pia ni mzuri kwa man to man football, tangia onyango anacheza Simba hawajawahi kula chuma 5 kutoka kwa Yanga.
Ukiangalia Cotton sports kwenye kombe la Mabingwa ukutwa wao ukiundwa na Che Malone wao ndio walikua timu ya Mkiani tena kwa kupokea vipigo vikubwa vikubwa tu leo uje uniambie ni beki kitasa Noop.
Shida mashabiki wa Tanzania hasa Simba na Yanga tuna mihemko sana na propaganda nyingi wakati mwingine tunajizima data kabisa na kusikiliza maneno ya kina Ally wote bila kuzifamu falsafa za mpira.
Roma ikisema imesema.