Cheating?!

THANSK mcd... MTALAAM WA TWANGA PEPETA
 
Au kwa mfano eti mtu anafiwa na mke wake baada ya miezi miwili mitatu kashaoa mwingine!!! Hivi kweli utasema amemuona huyo mwanamke na kumuoa mara tu baada ya kifo cha mkewe?

Hiyo haiwezekani wanakuwa tayari na uhusiano huko nyuma sasa wakishapata chance ya kuhalalisha ndo hayo yanatokea hata maumivu hayajapoa eti tayari mke ndani ya nyumba watu wanaroho ngumu aisee mie siwezi
 
Mmmmh! Haya maswali magumu jamani.
Kama ni mpenzi tu imetokea mmegombana ukiona hamna uelekeo unatoka tu na mwingine. Akirudi nitapima uzito wa ugomvi pia kuna time factor hapo. Kaugomvi kama wiki 1 tu ukakimbilia kwa mwingine hyo plan B itakuwa ilishaandaliwa zamani.
 
Inategemea ni mahusiano ya level gani,boyfriend and girlfriend,uchumba au ndoa?Katika swala la ndoa ni tofauti kwa mtazamo wangu maana pale inakuwa tayari mmeshaapa kuwa pamoja maishani mwenu,sasa hapo hiyo lazima itakuwa ame-cheat,lakini kama ni boyfriend na girlfriend aaaaah TUPILIA MBALI SIWEZI POTEZA MUDA,atakuwa hana subira huyo na sio mvumilivu
 
The Following User Says Thank You to MTM For This Useful Post:

The Finest (Today)​
 
Well said MTM and Biggie

St PM am waiting to hear from you
 

Kwamba kila mgogombana basi mtu awahi fasta kucheat? hapana....
Kama kila mmoja wenu anadhani mmeachana kwa ugomvi huo....mi sidhani kama yapasa kuitwa cheating....
 
Kugombana hakumaanishi kuachana
bado watu hao wapo kwenye mahusiano mwingine akifanya hivyo
atakuwa amecheat.
 
Ugomvi gani wa wiki moja kisha mrudiana? Wapenzi wa kweli hawalali bila kupata suluhu ya jambo linaloleta tofauti kati yao.
 
Mhhhhh!!!Kwanini mtu akae ndani akilia wakati kuna wengine wanamtaka?

Yaani umetoka kwenye kilio ghafla badala ya kutuliza akili ujue ni nini kikasababisha hicho kilio, na ujipange uhusiano ujao yasijekupata yaliokupata maana inawezekana kabisa hata wewe ulichangia kupata hicho kilio. mara umerukia kwa mwingine no lizzy hainiingiii akilini hata kidogo huo ni ukicheche kabisa na inawezekana huyo mliegombana ulikuwa humpendi ila ilikua bora liende na ulikua unacheat siku nyingi kwa kificho hapo umefunguliwa tu.
 
Definition yangu ya cheat ni kutoka nje ya mahusiano wakati ukiwa kwenye mahusiano mengine...km mtu kapanda juu na ikaonekana hafai kuplease basi decision yoyote itakayofikiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na mtu mwingine si kucheat huko,itakua kucheat kwa uliye nae kwa wakati huo km ulimpoka kwa mwingine asiye na mgogoro naye! Yametukuta sana haya!
 
Aliyekukimbiza mpaka ukajikuta kwenye mikono ya mtu mwingine ndo anaesuggest mrudiane!!Alafu sijaona mtu aliyesema kama atapenda aambiwe au mwenzake anyamaze!
 
Au kwa mfano eti mtu anafiwa na mke wake baada ya miezi miwili mitatu kashaoa mwingine!!! Hivi kweli utasema amemuona huyo mwanamke na kumuoa mara tu baada ya kifo cha mkewe?

Hehehe!Labda alikua anamfahamu tu!Kwa watu wengine kitendo cha mtu kukaa mwenyewe kwa muda mrefu baada ya kumpoteza mwenzake haina maana kwamba alimpenda sana!
 
MTM kwahiyo wanawake wakirudi ni sawa na kula matapishi eh?Na kwa wanaume je?Inawezekana mtu anakupa sababu ya kurudi...kama kuonyesha mabadiliko!Besides...kila mtu anastahili nafasi ya pili na kurudiwa ndo kunaweza kua nafasi ya pili yake!Mf. mzuri ni mwanamke/mwanaume aliyefanyiwa kitu kibaya kwa mara ya kwanza..ila kutokana na hasira hakutaka kubaki ili kujua kama itatokea tena au la!Baada ya kutafakari kwa muda akaona ampe mwenzake nafasi ya pili maana kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa
 
Kwamba kila mgogombana basi mtu awahi fasta kucheat? hapana....
Kama kila mmoja wenu anadhani mmeachana kwa ugomvi huo....mi sidhani kama yapasa kuitwa cheating....

Sio kila mkigombana ila ukifikia hali ya kumwaminisha mwenzako huna muda nae tena!
 
Ugomvi gani wa wiki moja kisha mrudiana? Wapenzi wa kweli hawalali bila kupata suluhu ya jambo linaloleta tofauti kati yao.
Raha kweli mapenzi ya aina hiyo!Hamna kununiana...ever!
 
mara umerukia kwa mwingine no lizzy hainiingiii akilini hata kidogo huo ni ukicheche kabisa na inawezekana huyo mliegombana ulikuwa humpendi ila ilikua bora liende na ulikua unacheat siku nyingi kwa kificho hapo umefunguliwa tu.
Hata kama haikuwahi kutokea kabla?Imagine mtu analia na akabembelezwa na rafiki yake ambae ni wa jinsia tofauti...bila kumbukumbu anajikuta wanaamka pamoja na kila dalili za kuhusiana!Kwanini asionekane kwamba situation ilimzidia!?
 
lizzy tujifunze kuappreciate yale tuliyonayo kutoka moyoni hata kama hatusemi,yatatupa wakati mzuri wa kutulia na kusonga mbele hakuna aliye mkamilifu kukamilisha maisha yetu ni kazi ya watu wawili kufanya mambo yakamilike kuliko kuhangaika na kuendelea kutafuta vitu ambavo ni incomplete.unaweza kuwa na mahusiano kumi ndio yakakamilisha unachotaka na wakati mwingine usikipate.tujifunze kuvumiliana na kupendana usiingie kwenye mahusiano sababu tu unataka kuwa na mtu.lazima uwe na sababu genuine kutoka moyoni ndio utakapoweza kumvumilia kwa hali yoyote.
 
Chauro ni wachache sana wanaoingii kwenye mahusiano wakiwa na malengo thabiti!Wengi ni kwa nia ya kutumiana tu kwa namna moja au nyingine ndo maana kila siku watu hawaishi kuimba wimbo wa 'majaribu'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…