Check engine light in Toyota Verossa

Joined
Feb 3, 2014
Posts
31
Reaction score
42
Habarini wakuu!! Ni matumaini yangu kuwa mko salama na mnaendelea na ujenzi wataifa!

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini hili jukwaa kuwa ni mahali sahihi kwa kupata elimu kuhusiana na vyombo vyetu vya moto lakini pia utatuzi wa changamoto tunazopata kwenye magari.

Gari yangu Toyota Verossa yenye injini ambayo ni 1G VVTI imewasha taa ya check engine napata Mashaka na wasiwasi pamoja na kuwa hakuna mabadiliko yoyote kwenye performance ya gari!

Hakuna mlio wowote tofauti na wa kawaida wala harufu yoyote!

Naomba wataalamu humu tujuzane gari inapowasha hii taa hasa kwa kesi hii ya Toyota Verossa ni sababu zipi kadhaa zinazoweza kusababisha hii taa kuwaka?

Na je endapo nitaendelea kuendesha hii gari pamoja na taa hiyo kuwaka nini kinaweza kutokea?

Natanguliza shukrani.
 
Inawaka kwa rangi gani? Kama ni nyekundu usiendeshe hiyo gari, tafuta fundi aje kuitengenezea hapohapo ilipo hata kama ni barabarani.
 
Fanya diagnosis mkuu..mambo ya check engine light si ya kupiga ramli...labda kama uwe na uhakika kuna kitu ulichomoa gari likiwa linawaka, hapo inaweza kufanyiwa reset
 
Check engine (yellow), mwaka wa 3 huu kwenye Toyota Harrier, mpaka nimeamua niizoee. Nilishawepelekea hao wenye diagnostic kits, wakanilia 50,000 zangu mara 3 na taa ikaendelea kuwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…