Cheka kidogo

Cheka kidogo

winston20

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2020
Posts
1,116
Reaction score
2,303
USILETE UTANI KATIKA MAPENZI

Mdada mmoja alitaka kujua kiasi gani anapendwa na mume wake, hivyo akataka kujua mumewe atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha!

Mwanamke huyo akaamua kuandika barua inayosema "Samahani mume wangu, nimeamua kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya mbali na wewe"*Barua hiyo akaiweka juu ya meza iliyokuwa chumbani. Baadaye jioni, muda wa Mumewe kurudi mwanamke huyo akajificha chini ya uvunguni wa wa kitanda mule chumbani Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma
kisha, akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua, halafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga milunzi na akiwa anavua nguo.

Akapiga simu na akasikika akisema hivi "hello mpenzi, nina raha sana leo.. yule mwanamke nuksi ameondoka mwenyewe bila kumfukuza nakutuachia uwanja, jiandae nakuja "Muda huo huo Mume akaondoka.~

Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa analia na kutokwa na machozi akaamua kutoka lakini amenyong'onyea na amelowa mashavu kwa machozi.

Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua mumewe aliandika kitu gani kwenye ile barua. Akakuta maneno haya "nimekuona miguu yako uvunguni tafadhali andaa chakula nina njaa sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia. Nakupenda mke wangu.

[emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hivi nani kampata mwenzakee
 
Back
Top Bottom