Kwenye hospitali ya vichaa,
mwandishi wa habari akamwuliza daktari:
"Wewe huwa unatambuaje mgonjwa huyu ni wa kulazwa, na huyu si wa kulazwa "? Daktari : Kuna njia nyingi.
Kwa mfano naweza kujaza maji kwenye sinki la bafuni, nikamwekea hapo kijiko cha mezani,kikombe na ndoo; Kisha nikamwagiza amwage maji yote yaliyo kwenye sinki.
Mwandishi: Bila shaka aliye timamu
atatumia ndoo.
Maana ndoo ndiyokubwa! Si ndivyo?
Daktari: Hapana! Mtu mwenye akili timamu atafungulia koki ya chini ya sinki. Tafadhali na wewe nenda kalale kitanda Namba-39. Nitakuja kuendelea
kukuchunguza zaidi! "
Hahhahaaa! Hivi kweli na wewe pia uliwaza ndoo?
Basi, kitanda chako ni Namba 40.