Chelsea kanimaliza

Deal28

Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
96
Reaction score
114
Wakuu chelsea ni chama langu ila kwa mwenenendo huu sijui kama nitafika, jana kanikata kila kitu kuanzia vibe hadi mtonyo nilimuamini sana nikamuwekea laki mbili duuh lakini kanibwaga.

Uchungu zaidi nilikoweka hata bonus hakuna , sijui ni wapi angalau ningepata kabonus kutuliza moyo, tuelekezane kidogo.
 
Kama unadhani unataka kukata tamaa basi muda wako bado. Imagine hawa jamaa walikuwa wanafanya mazoezi ili waishinde man city
 
Kwa hii Chelsea bora ifutwe tu. Mmarekani na siasa za ulaya zimetuharibia.
 
Pole. Usicheze kamari na pesa ambayo ikiliwa utaumia.
mimi niliamini kuwa ningetoboa lakini kilichonikuta duuh kama mimi laki mbili tuu kilio je wanaoweka milioni?
 
Uzi bila picha ni uhaya wa kishamba sana
 
mimi niliamini kuwa ningetoboa lakini kilichonikuta duuh kama mimi laki mbili tuu kilio je wanaoweka milioni?
pole, usicheze kamari kwa kiwango usichomudu kuhimili kikipotea.
 
we ndo wa kujilaumu,yaani timu inachezeshwa na kosi la pili na bado unaipa ushindi?kipindi chote hiki chelsea ako na rekodi mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…