Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Lampard alipotimuliwa na Chelsea mwezi uliopita klabu haikulipa mkataba wake uliobaki baada ya mabadiliko ya sera ambayo yalikuja baada ya kulazimika kutoa pesa nyingi wakati walimpomuondoa Jose Mourinho
Badala yake wameweka mshahara wake wa Pauni 75,000 kwa wiki kwenye muswada wa mshahara - na makubaliano ni kwamba ataendelea kulipwa hadi Julai ikiwa tu hatochukua kazi kwenye timu nyingine.
Na hiyo inamwacha Lampard katika nafasi ambapo ofa yoyote ya ajira inayokuja inaweza kumgharimu pesa nyingi.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42 anafahamika kuwa anafurahi kuchukua mapumziko kwa kipindi kifupi kufuatia kutimuliwa, baada ya kuwa na misimu mitatu yenye shinikizo kubwa tangu kuwa meneja huko Derby County.
Ingawa Lampard alikuwa na uwezo kuiendea ofa ya kukinoa kikosi cha Bournemouth lakini hakufanya hivyo kwa kuwa kwa sasa anatumia muda wake na familia yake.
Lakini pia ni ukweli kwamba kama angechukua ofa hiyo ingemaanisha mara moja pesa ambazo Chelsea inaendelea kumlipa zingekoma, ambayo ingemgharimu chini ya pauni milioni 2.