John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Chelsea imefanikiwa kubeba ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia baada ya kuifunga Palmeiras kwa mabao 2-1 katika fainali iliyochezwa Abu Dhabi, leo Jumamosi.
Mabao ya Romelu Lukaku na Kai Havertz yameipa Chelsea ubingwa huo wa kwanza kwao katika historia ya michuano hiyo. Bao la Palmeiras lilifungwa na Raphael Veiga.
Hilo ndilo taji pekee ambalo mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich alikuwa hajashinda tangu alipoanza kuwa mmiliki wa klabu mwaka 2003.