Chelsea yamfungashia virago kocha Thomas Tuchel

Chelsea yamfungashia virago kocha Thomas Tuchel

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Post-Image-1-4-scaled.jpg


Klabu ya Chelsea imemfuta kazi kocha wake Mkuu Thomas Tuchel kutokana na uwepo wa mwendelezo mbaya wa matokeo unaoikabili timu hiyo.

Kufurushwa huku kumetokea masaa machache baada ya kupokea kipigo cha goli moja kwenye michuano ya UEFA kutoka kwa Dinamo Zagreb.

Tuchel alijiunga na timu hii mwaka 2021 ambapo alifanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA) mwaka huohuo.

Kocha huyu ameondoka akiwa amecheza michezo 6 kwenye ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu huku akishinda mechi 3, droo 1 na kupoteza michezo 2.

Ameiacha timu hiyo ikiwa inashikilia nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi kuu ya EPL.
 
Mwaka huu changamoto
 
Chelsea imemfuta kazi Kocha Thomas Tuchel baada ya timu hiyo kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha tangu kuanza kwa msimu huu.

Chelsea ni ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa imecheza michezo 6 na kupoteza miwili huku ikianza vibaya Klabu Bingwa Ulaya kwa kufungwa na Dinamo Zagreb.

Tuchel aliwasili Stamford Bridge mwaka wa 2021 kuchukua nafasi ya Frank Lampard na kuanza vema kwa kushinda Klabu Bingwa Ulaya ndani ya miezi 6
 
Hahahahah uzuri wa haya mambo wakitaka kukuondoa lazima wakulipe na pia wakikubakiza wanakulipa.
 
Je wewe unaona nisahihi kwa kocha Tuchel kufukuzwa kama mdau wa soka
 
Haitawasaidia kitu chelnyeto msimu huu tutawachapa vitasa sana tu hamna timu
 
Kufukuzwa sindio kazi yao ndio maana JM alisema makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe
 
Sasa pamoja na usajili walioufanya Bado hawajiamini?
 
Back
Top Bottom