Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?


Unazunguka sana Kaka,
Iko hivi!
Kaka kakukopa NET 4,900
Dada Kakukopa NET 4,900
Jumla Una 9,800.
Umelipia Nguo 9,700 then ukabaki na chenji 100, then utata uko wapi hapo?
*
*
*
yaani katika alfu 10, umeigawanya kama ifuatavyo.
Nguo 9,700
Kaka 100
Dada 100
Wewe 100

Upo hapo??
 
9800 ni deni, na unapojumlisha na hela uliyonayo huwezi Pata 9900 Bali 9700 ambayo bado ni deni! Kiufupi ni kwamba huwezi jumlisha deni na hela ulonayo afu deni likaongezeka bali lazima lipungue maana utakuwa umepunguza hilo deni. Kwahiyo kitu unachokizungumzia wewe katika hesabu hakipo.
 
Bila shaka mmeamka salama wana jukwaa.
Nimeona si mbaya nikileta swali hili tukachemsha akili kidogo.

Juma alienda dukani kununua simu akaambiwa bei ni sh. 10,000. Bahati mbaya hakuwa nayo hiyo 10,000 ikabidi atoke nje akaazime 5,000 kutoka kwa Grol na 5,000 nyingine kutoka kwa Amos.
Baada ya kupata hiyo 10,000 Juma alirudi dukani kununua ile simu lakini akawa amepunguziwa sh. 300. Hivyo aliinunua kwa sh. 9700.
Sasa kwenye ile 300 ikabidi atoe 100 apunguze deni kwa grol na 100 nyingine kwa Amos. Hivyo alibaki na sh. 100 mkononi huku akiwa na jumla ya deni la sh. 9800.

Lakin sasa Juma akichukua ile 100 aliyobaki nayo akajumlisha kwenye lile deni lililobaki ambalo ni 9800 anapata jumla ya 9900.

Sasa naomba mniambie ile 100 ilipotelea wapi, maana nimeambiwa nikipata jibu napewa 25,000 asubuhi hii.
 
Kama aliuziwa simu kwa shilingi 9,700. Ina mana angehitaji kukopa shilingi 4850 kutoka kwa grol na 4850 kutoka kwa amos i.e (9,700/2 = 4850). Na kama yeye aliwapa shilingi mia kila mmoja ina maana so far ametumia 4,850 x2 +100x2=9,900. ukijumlisha na mia alobakiwa nayo yeye jibu ni buku kumi kamili.
 

Kwa mbaali nimekuelewa
 
Alipotoa 200 kwa ajili ya kulipa,alibakiwa na sh.100,Hivyo akawa anadaiwa sh 9800 kwa jumla..
Ukichukua deni(-9800) ukaongeza na sh.100 unapata 9700 ambayo anadaiwa.
Yaani -4900+-4900=-9800
-9800+100=-9700(Deni)
 

huwez kujumlisha pesa uliyobaki nayo katka jumla ya maden yako.hiyo mia moja uliyobak nayo ijumlishe katika kias ulichotumia wewe kununua simu ambapo utapata amount unayodaiwa.hakuna pesa imepotea.
 
huwez kujumlisha pesa uliyobaki nayo katka jumla ya maden yako.hiyo mia moja uliyobak nayo ijumlishe katika kias ulichotumia wewe kununua simu ambapo utapata amount unayodaiwa.hakuna pesa imepotea.

You might be right. Thank you
 
samahani kama swali hili lilishaulizwa kabla yangu.linasema hviii,
Nguo inauzwa shilingi 10,000/- nawe huna pesa ukaamua kukopa kwa dada yako shilingi 5,000/- na kwa kaka yako shilingi 5,000/- ukawa na hiyo 10,000/-
ukaenda dukani muuzaji akakuuzia kwa shilingi 9700/- na ukabaki na 300/-
kati ya hizo 100/-ukapunguza deni kwa kaka na 100/-ukapunguza deni kwa dada na kubakiwa na 100/-mfukoni.
baada ya kupunguza deni, dada anakudai 4900/- na kaka 4900/- ambazo jumla yake ni 9800/-
ukiongeza na ile 100/- uliyobaki nayo mfukoni inakuwa ni 9900/-
swali langu ni kuwa mia moja imepotelea wapi?
 
Hakuna mia iliyopotea kwa sababu hiyo mia ukiiongeza kwenye 9700 = 9800
 
Nguo ni sh 9,700 hivyo deni kwa kila mtu ni 9,700/2 = 4,850 na wewe umebakiwa na sh 100 ambayo ni sawa na sh 50@ hivyo deni ni sh 4,850+50 = sh4,900@ ambayo jumla ni sh 9,800

Huwezi jumlisha hela uliyolipa na hela unayodaiwa bado ukaita lote ni deni, ile sh 200 umeshairejesha hivyo haipo kwenye deni vinginevyo uwe umeamua kuchanganya historia na hisabati
 
Hakuna kilichopotea.
Chukua 100 yako ya mfukoni weka kwenye hela uliolipia kwa mangi, 9700, jumla itakua ni 9800, ambayo ni sawa na deni lako mpya unalodaiwa.
Ukitaka ije 10,000, chukua ile 200 uliowapatia daka na kaka yako, kila mmoja mia mia. Hio 200, ukiweka kwenye deni lako mpya, 9800, jumla itakua ni 10,000, sawa na deni lako la zamani.
 

kumbuka, ulikopa 10,000 (dada 5000 na kaka 5000). uliporudisha 100 kwa kila mmoja ikawa umekopa 4900 *2 =9800
so jumla umekopa 9800 lakini nguo inauzwa 9700, kwahiyo kuna chenji ya sh 100 hapo.
kwahiyo, 9800 + 100(uliobaki nayo) + 100 (checnji ya kwenye kununua nguo) = 10000
100 ni chenji ya kununua nguo 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…