Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Mods, mukiona inafaa muiunganishe na thread ile kuu.
waendesha mashitaka leo wameongeza shitaka la kuendesha gari lisilokuwa na bima katika mashitaka yanayomkabili Chenge kwenye ile kesi yake ya kuua watu wawili aliowagonga katika Bajaj.
Pia, Majid Gharib, yule mmiliki wa bajaj ambaye alikimbia, naye ameongezwa kwenye kesi hiyo
Ameshitakiwa kwa kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva wakeMajid Gharib, yule mmiliki wa bajaj anakosa gani huyu?
Ameshitakiwa kwa kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva wake
Ukiangalia unaweza kubuni kuwa Chenge huenda akakwepeshwa na mauaji na kuhukumiwa kwa hili la kuendesha gari bila ya bima na yule mmiliki wa Bajaji kutolewa kafara.
Du kumbe nalo ni kosa????
Mimi naona kuliko kuzugana kila siku, Chenge wamwachie tuu ili aendelee na majukumu yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama kitukufu na kama kuna uwezekano arudishiwe ule wadhifa wake wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali maana toka aondoke ofisi ile Michongo imepungua na visenti havipatikani kwa wingi.
Sh..xyz taip...
Ameshitakiwa kwa kushindwa kutunza kumbukumbu za dereva wake
Kwa asiye fuatilia mwenendo wa siasa za jamuhuri ya Danganyika atashtushwa na hili. Sisi wengine tuliisha acha lipite kama mengine mengi (mazito zaidi) yalivyopita. Sioni umuhimu wa kupoteza muda wa mahakimu kwa huyu mhe. vijicenti (wakati mwisho wa hili unajulikana), nawasihi mahakimu waendelee kusikiliza na kuhukumu kesi za walalahoi kuibiana vijisimu kariakoo na mbagala!
Huyu ndiye mwenyekiti kamati ya maadili wa CCM, vioja vitupu!!
CCM nambari one
Du, Bongo ni nchi nzuri sana.... hivi kesi kama hii ingemkuta mshkaji tu wa street angekuwa wapi saa hizi? Haya mambo kuna haja ya kutoyafuatilia kabisa maana saa zingine roho inauma mno inatamani ipasuke! Hapa tayari mchongo unachorwa na mzee atahukumiwa kulipa fine kwa kuendesha gari bila bima na kufungiwa leseni miezi miwili, kwisha kazi! Kwa sasa habari kuwa alikuwa amelewa hazisemwi tena, any way tunamuachia Mungu maana nae ana majibu yake, kesi ya Dito iligeuzwa ikawa bila kukusudia ili hukumu iwe kifungo cha nje lakini Mungu nadhani alichoka na ujinga huu.......
Mjadala huu wote wa nini?
Hamjui kwamba viongozi mliowachagua si Chenge pekee bali nina maanisha wote mliowachagua kama viongozi wenu( hapana nina maana watawala wenu) at the same time mmewapa tiketi ya kuwaueni, tena kuua yeyote kwa namna yeyote bila kesi?
Hadi pale wadanganyika tutakapokuwa tumejua kuwa tuko katika utawala mbovu sana tangu uhuru yaani utawala usiokuwa wa sheria kwa wakubwa lakini ni washeria kwa wadogo, hapo tutakapokuwa tumeamka katika usingizi huo, hapatatokea uvunjifu wa sheria wa viongozi wetu kwa dharau kubwa kama ninayoiona sasa hivi.
Lakini wasubiri tu iko siku watu wanachoka na mbaya inakuwa mbaya.
Siku akijaribu kuua ndugu yangu sikubali mambo ya kusafirisha maiti wala pesa ila nami namvaa mbaya iwe mbaya. Tena sintajali ni nani na ana wadhifa gani. Lazima nimuwinde nijilipize kisasiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii wamezoea sana sasa. Tena wameifanya fashionSawa lakini wanapaswa kuelewa kuna nchi wanapaswa kuiongoza na watu wa kuwatumikia, ile ole wao siku isiyo na jina inakuja, wala haiko mbali!