Chenge Joka la Makengeza v/s Kakobe katiba mpya

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana JF,

Angalia hii:

"Mwandishi Mkuu wa Katiba Pendekezwa, yeye mwenyewe amesema anapenda aitwe JOKA LA MAKENGEZA! Niliposikia juu ya Jina lake hili, nilipigwa na butwaa! Katika Biblia, Joka ni Ibilisi au Shetani (UFUNUO 12:7-9; 20:1-2), maana yake ni kwamba Mwandishi Mkuu wa Katiba Pendekezwa, ni Joka yaani Shetani, na hivyo tunaweza kusema Katiba hiyo ni ya Kishetani, maana imetokana na Shetani ambaye ni Joka lililoko kuzimu! Kumbe basi, siyo tu kwamba Katiba Pendekezwa imeahirishwa, ila ni kwamba Mungu ameikataa tangu siku ya kwanza ya mchakato wake! Kwa sasa tuwaze tu kujiandikisha kwa wingi katika Uandikishaji wa Wapiga Kura, kwa BVR, na kuwa tayari tu kwa Uchaguzi Mkuu, na kuisahau kabisa Kura ya Maoni.
 
Mungu unayemtaja wewe hadhihakiwi hata kidogo usituchanganye hapa, kama huna hoja umeishiwa useme upate msaada, Hakuna mwandishi Mkuu yeyote anayemiliki Katiba acha uongo mchana kweupe Katiba inayopendekezwa ni ya wananchi wenyewe na chonde usimsingizie Mungu kuwa kaikataa, kuahirishwa tarehe ya kufanyika kwa jambo fulani mbona kawaida tu, kupanga ni kuchagua wewe una mambo mangapi umesogeza mbele, ukute hata harusi yako uliisogeza mbele leo unajifanya kutupa red writings ili sijui tuogope, acha kujilisha upepo na kukimbilia Tarshishi kama Yona rudi Ninawi unatakiwa kuijenga nchi yako wewe mwenyewe, usiwe nabii wa Uongo muda wa kazi hiyo umeisha, Watanzania wako makini na wanaendelea kufuatilia kwa makini issue ya katiba ili waipigie kura kuipa ridhaa!!! Ha ha ha ha utakalia kushangaa kama wale wanawali wapumbafu kwenye Biblia waliokwenda kumlaki Bwana Harusi usiku huku taa zao hazina mafuta wakitegemea kwenda kununua akifika matokeo yake wakajikuta wamechelewa mlango ukafungwa. Ushauri wangu kwako jihadhari sana kuwa nabii wa uongo!!!!
 
haaa!!!!!!!! kumbe na wew ni mjumbe wa shetani?!!!!!!
 
Usimdhanie mtu kama utakavyo wewe. Wajumbe wowote huwa wanatabia ya kujuana , kama claudiaeliakimu ni mjumbe wa shetani nawe pia ni mjumbe kwa sababu unamjua huyo shetani. Huwezi kusema kitu usichonacho.
 
Back
Top Bottom