Uhusiano upo, hii maana yake kuwa ana aleji na hivyo vitu hivyo ili kuepusha madhara zaidi ni bora akaviacha kabisa. Nimeishaona watu wengu wenye aleji na hiyo gold ya kuchovya lakini mara tu baada ya kuacha na tatizo linakwisha lenyewe ila kuendelea kung'ang'ana navyo kisa urembo ataja rembeka asivyopenda.
Nina rafiki yangu mmoja yeye alikuwa na tatizo kwenye masikio yalivimba vile vinundu mara tu baada ya kutobo. akafanyiwa operation wakavikata akafikiri tatizo nalo limekwisha akawa anavaa hizi hereni za kuchovya na nyinginezo na akaja toboa tena vitundu vingine viwili kwenye masikio muda si mrefu alikotoboa, alikofanyiwa operation kote vinundu vikavimba kama ndio alitia mbolea. Bahati nzuri alimpata daktari mzuri akamfanyika operation nyingine ila akamwambia kama atakuwa ana uwezo wa kuvaa pure gold masikio yakipona baada ya operation aende akamtoboe na awe anavaa pure gold akaona hatakuwa na huo uwezo uwezo wa kuvaa pure gold. hivyo baada ya kupona hakutoba tena masikio ila siku hizi ameamua kuvaa hereni za kubana naona hizo hazimzuru.