Chereko,chereko

Msindima

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2009
Posts
1,018
Reaction score
35
Habari zenu wana jamii forum
Napenda kuwajulisha kuwa nategemea kufunga harusi mwezi ujao,hivyo mimi nikiwa member wa forum nimeona sio vizuri kuwa kimya bila kuwajulisha wana-jamii.
Naomba pia mnisamehe kwa kuchelewa kuwahabarisha ni majukumu ya hapa na pale.
Mungu awabariki,nawakaribisha sana.
 


karibu kwenye game mrembo, nakutakia kila la kheri, mchele wapi sasa mami na mie nije nipige vigelegele.....
 
Hivi ni kufunga harusi au kufunga ndoa?
anyway. wewe Msindima ni He au she?
Hongera sana ndugu yangu, kila la kheri karibu katika ulimwengu wa Ndoa.
 
A slippery of the tonque ni kufunga ndoa then baada ya hapo ndo atakuwa na kashere/harusi/reception.
Karibu kwenye hili chama la Mr and Mrs.
Tuko pamoja
 
Huku ni patamu ila pana majaribu yake yataka moyo,karibu sana
 
Maandalizi mema na kila la kheri kwenye ndoa yako..Hongera!!
 
Hongera,muwe mnatuwekea na photos kule kny jukwaa la photos basi...
 
Hongera,nakutakia harusi njema na ndoa ya furaha...........msisahau KUSALI.Shetani huwatamani sana wana ndoa ili awavuruge.
 
Wow..hongera sana Msindima kwa hatua hii...tupo pamoja sana

hebu tuambia harusi itakuwa wapi exactly ili kama tunaweza kukusindikiza tuje,
 

hongera ni jambo zuri tupo pamoja na weka wazi ili tuweze kushiriki kwa namna moja au nyingine
 
Karibu sana!

Huku ni raha mtindo mmoja ilimradi ujue kula na kipofu! teh teh teh
 
Hivi ni kufunga harusi au kufunga ndoa?
anyway. wewe Msindima ni He au she?
Hongera sana ndugu yangu, kila la kheri karibu katika ulimwengu wa Ndoa.

amekosea kidogo ni kufunga ndoa,

Hongera sana msindima kwa kuamua kuhalalisha uhusiano wenu, tupe venue tuje tushereheke pamoja nawe!
 
Wow..hongera sana Msindima kwa hatua hii...tupo pamoja sana

hebu tuambia harusi itakuwa wapi exactly ili kama tunaweza kukusindikiza tuje,

Ok Kaizer,send off pamoja na harusi vitafanyika Arusha.
 
Hongera sana Msindima mungu akutangulie katika siku hii muhimu kwako ...
 
Wow..hongera sana Msindima kwa hatua hii...tupo pamoja sana

hebu tuambia harusi itakuwa wapi exactly ili kama tunaweza kukusindikiza tuje,

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi nawafahamisheni kuwa tukio hili la kihistoria litafanyika ARUSHA

Kwa anayetaka kuhudhuria anitafute kwa PM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…