Cheti cha ndoa

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
6,324
Reaction score
2,240
NDOA bana ajabu kweli.
Ndoa ni kama shule,mara nyingi kabla ya kuingia kwenye ndoa sio rahisi
kumfahamu mwenzako kwa kila kitu,hasa tabia zake zote.

Kwa kua ndoa ni kama shule,tunategemea kila siku inavo ongezeka unazidi
kumuelewa mwenzako zaidi na zaidi,lakini shule hii ni ya ajabu sana.

Tofauti na shule zingine ambazo unapata CHETI baada ya ku-graduate,..
shule hii ndiyo pekee ambayo mtu anapewa CHETI wakati ndio kwanza anaanza shule yenyewe.

Ni nini maana haswa ya cheti cha ndoa?
Umefuzu nini hadi upewe cheti cha ndoa?

Je,ukivunja ndoa,ukafunga nyingine,ukavunja tena na tena na tena na tena
na hatimaye ukawa na vyeti 10,..........Unastahili kutunukiwa cheti kingine kama masters hivi au?
 
I can calculate motion oa heavenly bodies not the madness of pipo, sijui ni newton au albert einstein alisema.
 
I can calculate motion oa heavenly bodies not the madness of pipo, sijui ni newton au albert einstein alisema.

Awapi,...hii niyako peke yako.
Newton na Einstein hawakuwahi kujua kiswanglish hata sekunde moja.
 
Cheti cha ndoa ni taratibu tu kuonesha mmefunga ndoa na hakina maana zaidi ya evidence(ushahidi),na kisheria sio kitu cha msingi kama ndoa yenyewe ndio sababu kuna mazingira hata bila hicho cheti mnatambulika kama wanandoa kisheria(kwa mfano customary marriages na hata under the presumption of marriage-hapa nadhani wanasheria watanielewa zaidi).

Na ukiachana basi hicho cheti cha ndoa hakina thamani zaidi ya ushahidi tu kuwa there was once a marriage..labda sanasana ‘talaka‘ ndio inachukua thamani ya cheti cha ndoa wakati huo.

Na kwa kuwa cheti cha ndoa sio ndoa bali ni ushahidi tuu hakuna cheti cha uzamivu wala uzamili-haileti maana yoyote wala haiongezi tofauti yoyote!
 
huwezi pewa talaka kama huna cheti cha ndoa, kwahiyo cheti muhimu sana, ukiwa na cheti rights zako katika ndoa zinakuwa recognised zaidi than presumption of marriage' kumbuka presumption of marriage does not legalise marriage, is still a presumption' can be rebutable. cheti muhimu sana...ingawa ndoa sio shule, ni mtihani, shule iikuwa u-boyfriend na u-girlfriend,
 
Je,ukivunja ndoa,ukafunga nyingine,ukavunja tena na tena na tena na tena
na hatimaye ukawa na vyeti 10,..........Unastahili kutunukiwa cheti kingine kama masters hivi au?

kuna zawadi wa kufanya vibaya kama kwenye Holywood huziita.........the Razzie........the worst performing actress or actor is........labda hii itamfaa mhusika......
 
Mwenza mzuri kwenye mahusiano atakuwa mwenye PhD au post doc ya ndoa. Huyu anajali na kujijali.

Usianzishe mahusiano na asiyejua ndoa, hana experience.
 
Mwenza mzuri kwenye mahusiano atakuwa mwenye PhD au post doc ya ndoa. Huyu anajali na kujijali.

Usianzishe mahusiano na asiyejua ndoa, hana experience.

Utajuaje ana experience?
Akisha achana na mwingine kisha akakupa CV yake sio?
Maana kama mwenye experience ni aliye kwenye ndoa huwezi mpata maana
busy na ndoa yake.
 
Utajuaje ana experience?
Akisha achana na mwingine kisha akakupa CV yake sio?
Maana kama mwenye experience ni aliye kwenye ndoa huwezi mpata maana
busy na ndoa yake.

huwezi pata vyeti vingi vya ndoa kama uko na ndoa moja kwa mazingira ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…