Chezea Abedi, ..utadedi!

Chezea Abedi, ..utadedi!

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
Mshua kagomakabisa nisitinge Loliondo, kila nikimstua ujue ananipa zipi? Niweiti mpaka amalizane na projekti flani ambayo inamfanya awe bize sana.
Sasa basi...

Washua kama hawa ujue ndio unajikuta unatoroka unaibuka kwa Pasta kwa kujiiba nini, unaenda kukumbana na mshua naye yuko kwenye foleni ya Ze Kap, sijui unafanyaje hapo kudadadadadeki.
Ukisikia mambo ya ngoma droo ndio hayo!

Niaje wazeiya?
Kitaani kwangu bwana, masela wengi ni mahom'boi ujue, wengi wanaishi kwa maza nini na famile kwa ujumlakwa hiyo suala zimala wageni, hasa wa diferenti seksi, a.k.a jinsia pinzani, huwa tunategemea sana ghetto la mtu mzima Muddy, ndio watu tukarekebishie mambo yetu yale.
..umenisoma?

Asa kumbe mchizi bwana ukizama tu anakuwa anakulia deo ishu nzima unayokuwa unapiga kama umekuja na shori wako nini, jamaa anakula chabo mwanzo mwisho, halafu kamasiku imetokea mmezinguana anakuchana kwamba mtu mzima umeingia na kitu ghetto hujakamua nini, ..unaanza kujiuliza kajuaje?
Jibu likawa halipatikani!

Si unajua masela wakiamua lao, wakahisi tu kwamba inawezekana mwana anatuliaga chapo, kwa hiyo tulihamishe goma, tusije na wageni mchana, ngoma iende naiti, watu wakakubaliana, wakikokota magoma yao kitaa wanayaingiza naiti kwa Mzee Muddy, tukamuona kama kakosa raha hivi, ila ze dei afta akaja na mpya.
Uliza ipi?
Eti swichi ya taa ya ghetto imeharibika kwa hiyo taa haizimwi ukizima taa unampa tabu mida mida sababu inakuwa kama inaleta shoti hivi...
Dah!
Masela wakajibu Poa, wakaanza kuibuka hivyo hivyolakini kuna mwanangu mmoja hivi anaitwa Abedi ni mtata kupitiliza unaambiwa, mzinguaji kupita kiasi kudadadeki kitaani unaambiwa tukiwa na ishu iliyoshindikana watu wanamtafuta Abedi wanamkabidhi mchongo amalizane nao, ..si komandoo?
Basi bwana, Abedi akaitwa, akapewa mpango mzima!
Sasa Abedi sijui ana dharau?

..akawa anacheka cheka tu wakati tukimpa mchongo. Tulipom'bana akatupa mpango mzima kwamba hiyo ishu yeye mwenyewe ilikuwa inamzingua longtime na alikuwa anatafuta baraka za maskani ili amuoneshe mwana kwamba anachokifanya si tunakinya..... tunakinyaka sio, ila tumeamua tu kuuchu... kuuchuna tu!
Watu wakamkodolea, mastamaindi wetu, tukaanza kumuuliza inakuwaje?
Akatuambia wanangu tulieni mi nalirekebisha hili suala mbona fasta tu?

...ngojeni!
Mchizi pale pale unaambiwa akainua waya, akamvutia demu wake flani hivi wa mitaa ya Gomzi, akamwambia aibuke mitaa ya kwake, ana ishu muhimu sana anataka mpe, mademu si unajua tena akisikia sauti ya jeba?

..Jeba limeita tena?
Mbona dakika stini nyingi, demu akavuta waya kwamba yuko maeneo!
Uliza saa ngapi sasa hiyo mwanangu mwenyewe? Kama moja moja jioni hivi ilikuwa inaaprochi, Abedi akamuibukia Muddy, akamuomba funguo mchizi akampa, ila Abedi sasa akataka mengine.
Akamuuliza kama atakuwepo araundi au ana misele?
Mchizi akajibu ana mchongo wake uko kino anaenda kufuatilia angerudi leiti sana, kama tano moja hivi, abedi akajibu poa, akasepa zake, akampokea demu wake, akaingizana naye Magetoni!
Mwanangu eh, ilivyoishia neksti wiki ntakupa au vipi?
..
 
Ivuga mbona hiki kiswahili chako cha kisela zaidi????????

natoka!! ngoja niwasubiri wasela nione wanaanzaje kwanza!
 
Hiyo uliyotumia ni lugha ya kiswahili kweli au kichinaswahili, kwani hata kiswaingilish hakipo.
 
Ngoja jini mahaba lisikie haya mambo mi simo ngoja niwahi south
 
Mh kuna mtu kaiba password ya ivuga leo au kaka umepuliza kitu toka arusha leo mwe!
 
we bwana mdogo nikikukamata, utanisoma vizuri, kiswahili gani hicho unatumia? nyie ndo mnaoharibu kiswahili chetu nyie...
 
Ivuga, gud writing. Napenda utofauti kama huo wa uandikaji, yani kama vile umetukua maskan unatupa mchongo. Mi nakusubiria hadi nikuone umeweka kituo kikubwa ndiyo nitasepa.
 
mambo ya JIMMY wa mwananchi newspaper:juggle:
 
Mi nahisi Ivuga na Fidel leo kuna mtu anatumia I'd zenu, sio bure aisee!!! Au mmekunywa nini?
 
safi sana Ivuga,mtu unatakiwa umudu mae4neo yote!!!
 
Daaah stori ya skani la machizi ipo mwake kinoma! Ngoja nipindue, nikirudi nicheki sanga la chabo kwa mtata Abeid limeishaji!
 
Back
Top Bottom