Chia Seeds - Kilimo na Masoko

Joined
Jan 10, 2018
Posts
44
Reaction score
55
Baada ya kujua manufaa ya Chia seesds nimeasmua kufanya majaribio ya namna ya kuzilima. Nimeanza na eka moja.
Nimeshindwa kutafsiri maelezo haya kwa kiswahili, lakini kwa ufupi hii ni lishe iliyomo kwenye Chia seeds, Waweza pia ku-google Chia seeds:

Chia Seed Nutrition Profile

The reason chia seeds are so beneficial is due to them being rich in fiber, omega-3 fats, protein, vitamins and minerals.

For example, one ounce (28 grams) of chia seeds contain about: (1)

  • 137 calories
  • 12.3 grams carbohydrates
  • 4.4 grams protein
  • 8.6 grams fat
  • 10.6 grams fiber
  • 0.6 milligram manganese (30 percent DV)
  • 265 milligrams phosphorus (27 percent DV)
  • 177 milligrams calcium (18 percent DV)
  • 1 milligram zinc (7 percent DV)
  • 0.1 milligram copper (3 percent DV)
  • 44.8 milligrams potassium (1 percent DV)
Chia seeds also contain essential fatty acids alpha-linolenic and linoleic acid; mucin; strontium’ vitamins A, B, E and D; and minerals, including sulphur, iron, iodine, magnesium, manganese, niacin and thiamine; and they’re a rich source of antioxidants. Soma 9 Chia Seeds Benefits, Chia Side Effects + Chia Seeds Recipes - Dr. Axe
Naambatisha picha za mwanzo wakati zimeota, ikiwa ni wiki tatu baada ya kupanda
 
masoko ya uhakika?
natafuta soko la uhakika. Ilikuwa vigumu kutafuta soko wakati huna product hasa product kama hii ambayoi ni mpya.
Kulingana na manufaa yake nafikiri somo litapatikana.
Mbegu mimi niliuzia na rafiki yangu kwa shs 10,000 kwa kilo, sijui yeye aliziapta wapi ila baada ya kuvuna nitakuwa na mbegu za kutosha. Japo mimi nilivyopanda ni kama zilikaribiana sana, lakini nadhani kilo moja inaweza kupanda eka moja.
 
Kwa sasa (wiki tatu baada ya kuanza kutoa maua) zimeanza kukomaa, hivyo anayehitaji kununua tuanze kuwasiliana humuhumu
 
Zinahusika na nini hizi mbegu
Hizi mbegu zina viini lishe vingi kwa manufaa ya binadamu, Kwa bahati nzuri nimepata maelezo kwa kiswahili kutoka https://www.facebook.com/ kama ifuatavyo

Matumizi na faida za Chia Seeds.

(- High Fiber content promotes longevity, Omega 3 fatty acids
- Omega 3 Fatty acids for heart functioning and reduce aging acceleration symptoms, contains high antioxidants, energy builder, mantains normal blood sugar abd pressure, improve sleep)

- Inasaidia moyo kufanya kazi yake vyema na kuzuia matatizo yatokanayo na umri unavyosogea.
- Nafaka iliyomo ndani mbegu za Chia inasaidia kufufua seli za mwili na kuziimarisha
-Chia seed inasaidia kusaga chakula katika kiwango kile kinatakiwa na mwili
-Chia seed inaimarisha kinga ya mwili na kukukinga na marathi nyemelezi
- Chia seed inakupa nguvu mwilini
- Inasaidia wenye shida ya sukari na pressure

- Inasaidia kukupa usingizi mzuri
- Inaondoa shida ya tumbo hasa wenye shida kwenye usagajiwa chakula na kutokupata choo
- Chia seed inachoma mafuta magum ya tumbo hivyo itakusaidia kupungua na kuwa imara zaidi

Matumizi
-Asubuhi kabla ya kula chochote weka vijiko viwili vya chakula kwenye kikombe weka maji ya moto ukipenda kamulia limao. Kunywa mchanganyiko huo. Itakupa nguvu na kukushibisha kunywa chai yako baada ya nusu saaa au zaidi.

-Unaweza pikia kwenye chakula chako kama mchuzi wa samaki nyama au kuku
- Inafaaa kuchanganya kwenye uji ,maziwa ,juice maziwa mgando, smoothies, fruit salad, vegetable salad etc
- Unaweza nyunyiza juu ya chakula chako wakati wa kula kama wali ndizi supu etc
- Unavyozidi kutumia ndivyo matokeo utaona kwa haraka
-Chia ni chakula muhimu na adimu sana. Tumia Chia Seeds upate kinga ya mwili imara uepukane na magonjwa sugu.
 
Ngoja Nijifunze zaidi juu ya zao hili geni kwenye upeo wa macho yangu na masikio pia.
 
Nimepokea simu nyingi sana na kwa kweli nyingi sikuwa na majibu kamili kwa kuwa nami ni mara ya kwanza nalima zao hili. Sasa najiandaa kuvuna, baada ya hapo nitakuwa na majibu mengi.
Asanteni sana na tuendelee kuwasiliana.
Naambatisha hali ya shamba kwa sasa (settings za kamera mwanangu alizibadilisha - hiyo tarehe ni 10.2.2018 siyo 10.3.2018
 
Mbona zimekauka mapema sana??

Yaani zao unavuna ndani ya mwezi mmoja??

Umelimia wapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…