Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
"CHICKEN ON THE BONNET" (KUKU JUU YA BONETI YA GARI)
Hawa kuku wawili nimewaona wamepanda juu ya boneti ya gari nje ya nyumba yangu.
Nikawa naomba dua wasiruke hapo kabla sijawapiga picha.
Picha kama hii huwezi kuipata hata kwa miaka mia.
Haraka nikaingia kazini na nikapiga picha nikianza kwa mbali ndani kwenye Majlis yangu kwa hofu kuwa nikiwakaribia watakimbia.
Taratibu nikawa nawasogelea hadi kutoka nje na kuwapiga kwa karibu.
Nadhani waliponiona niko karibu na wao ndiyo mmoja akaruka chini kisha mwenzake akamfuata.
Kuku hawa wamenikumbusha Arusha mjini karibu ya soko kuu kwenye Nyama Choma Maarufu ya Khan.
Hakuna mtu Arusha ambae hapajui mahali hapa lakini naamini ni wachache sana wanajua jina la Nyama Choma hii.
Naamini mimi ni mmoja wa watu wachache wenye kujua kuwa hapa panaitwa, "Chicken on the Bonnet."
Nilijuaje?
Nimetoka Tanga nilipokuwa nafanyakazi nimekuja Arusha kwa shughuli za kazi.
Zaidi ya miaka 20 imepita sasa.
Jioni jua limetua nikakodi taxi kwenda mjini katikati nikamwambia dereva wa taxi anipeleke sehemu ninayoweza kupata chakula kizuri.
Yule dereva wa taxi akanitazama.
Nilikuwa nimevaa kanzu.
''Jinsi ninavyokuona nitakupeleka mahali naamini utapapenda.''
Akanifikisha kwa Khan.
Hakika nilipapenda hata kabla sijaonja chakula chake.
Hii nyama choma iko katikati ya mtaa na mchana ni duka la spea za magari usiku duka likishafungwa hapo barazani na nishemu kubwa panapangwa majiko, meza na viti.
Kuna meza ndefu imesheheni mabakuli ya kila aina ya salad kuanzia karoti, pilipili, vitunguu maji, chachandu za kila sura na kila aina zenye pilipili moto na baridi, ukwaju, mikate ya ajemi ya ''plain'' na ya vitungu saum ili muradi kazi ni kwako mlaji.
Pembeni ndipo yapo majiko yenye kuku wa kila aina, nyama, sheesh kabab nyuma yake wamesimama wachomaji nadhifu kwa mavazi, tabia na lugha.
Niliposogelea pale Khan akanikaribisha.
Alikuwa hajapata kuniona na mara moja akatambua mimi ni mgeni.
Hapo ndipo ulipoanza urafiki wetu uliodumu hadi leo.
Sifiki Arusha lazima niende kula chakula cha usiku kwa Khan.
Khan anaendesha biashara hii na ndugu zake wa kiume na ndiyo wanakuwa hapo kuchoma nyama na kuhudumia wateja kwa jumla.
Kuna vijana wote wamevaa unifomu nadhifu wako kazi yao kuhudumu.
Khan akanizungusha kwenye yale mabakuli ya salad mezani kunionyesha na kunieleza mna nini ndani.
Hapa ilikuwa baada ya mimi kufanya oda yangu ya chakula.
Nakumbuka tulipofika sehemu ya pilipili akaniuliza kama napenda pililipi.
Hapo ndipo akaanza kunipa darasa la zile pilipili akinitahadharisha wapi nitie mkono kama mpenzi wa pilipili na wapi nikae mbali napo kama sina nguvu ya kula pilipili.
Khan akanieleza kuwa hivyo vyakula vyote vinatengenezwa na wake zao.
Khan akanieleza kuwa sehemu hii imeorodheshwa New York Idara ya Utalii kuwafahamisha Wamarekani wanaokuja kutembelea Tanzania wasikose kufika na kuonja jiko la Kitanzania na wamesajiliwa kama, ''Chicken on the Bonnet.''
Jina hili linatokana na mandhari ya mahali pale kuwa ni sehemu iliyo wazi unaiona mbingu na unapigwa na upepo huku unakula chakula chako.
Kuanzia siku hii Khan akawa rafiki yangu na kila akiniona nimefika pale atanisalimu kwa kusema, ''Karibu Mzee wa Tanga.''