Chid Benzi aswekwa lupango kwa kumjeruhi mwanamke

michepuko

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
1,192
Reaction score
345
Ilikua siku ya jumapili ya pasaka majira ya usiku,katika maeneo ya ilala corter,ktk baa ya Ngudu opposite na corter za national housing ilala,
Ndipo kulitokea kutoelewana kati ya Chid benz na dada mmoja inayesemeka ni mtu wake wa karibu aliyefahamika kwa jina moja la Aisha,Chidi kwa hasira alimporomoshea kipigo kikali Aisha na kupelekea kumngoa meno na kushonwa yuzi 6 kunako hospital ya amana ilala.
Chid benz alisekwa ndani ktka kituo cha polisi ilala mpaka siku ya jummanne na kulazimika kuvuliwa kipini chake cha pua kwa kashfa nzito kutoka kwa polisi waliokua zamu siku hiyo.


 
Ukiona mwanaume anampiga mwanamkee ujue huyo mwanaume ni muoga pia hajiaminiii
 
Kufulia kbaya jaman, stress za kushuka ki mzki znampeleka payaya ss
 
Now I am certain why I never liked this guy.

He has no style.
 
ATUPWA MAHABUSU Habari zimeeleza kuwa, Chid alipofika kituoni kwa ajili ya kutoa taarifa, alidakwa na kusokomezwa mahabusu kwa vile tayari alikuwa ameshafunguliwa mashitaka. Chanzo kilichopo polisi hapo kimeliambia Amani kuwa, jamaa alipoambiwa avue mkanda ili atupwe sero alileta ubishi hivyo kusababisha polisi watumie nguvu ya ziada kumdhibiti kwa sababu alisema yeye ni mtu maarufu hivyo hawawezi kumtisha. AKUTWA NA BANGI Wakati msanii huyo anayesifika kwa sauti nzito akitaka kuingizwa ndani, alisachiwa na kukutwa na misokoto miwili ya bangi hivyo kuandikishwa kesi nyingine ya madawa ya kulevya mbali na ile ya awali ya kujeruhi.
 
Nlishtuka nikajua kawa punda kumbe ni misokoto miwili ya bangi mbona maelezo yake madogo tu kua ni dawa ya degedege anampelekea mwanawe.
 
Polisi wa Tanzania siwaamini hata kidogo, hasa ukiwa hapo kituoni, hizo kesi za bange unapewa tu.
 
Nlishtuka nikajua kawa punda kumbe ni misokoto miwili ya bangi mbona maelezo yake madogo tu kua ni dawa ya degedege anampelekea mwanawe.

duu kwenye gari ninayo sita na ofisini minne sijui nikaisalimishe au nikajisalimishe?
 
Kumbe Bangi,
Ile si madawa ya kulevya, ule ni mmea
 
Mi Police Walinisingizia Nimekamatwa na Bangi hivi hivi !
 

Bangi siyo madawa ya kulevya kwani kule Iringa na Njombe wanatumia kama mboga ya majani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…