Chidi Benz ahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo ametoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini kwa rapper, Chidi Benz.

Chidi alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kusomewa mashtaka matatu ya kukutwa na madawa ya kulevya mwaka jana. Alikuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili wasiokuwa na hatia.

Faini anayotakiwa kulipa ni shilingi laki tisa. Chidi alikutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 38,638, na bangi yenye thamani ya shilingi 1,720 pamoja na na vifaa ya kuvutia dawa hizo ambavyo ni kijiko na kigae.

Tukio hilo lilitokea October 25 mwaka jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya kwenye show.


Chanzo: bongo5
 
laki tisa hana huyo labda achangiwe na mateja wenzake akina t.i.d
 
hizo inabidi alipiwe na mashabiki wake labda
 
Nita muona mpumbavu akienda jela kwa faini ndogo kiasi hicho... Nikama wame msamehe tu sema kama mtu ukishindwa kuelewa mchezo uta kimbilia jela.... Pole lakin bro.. nilisha wai kulala lock up kwa lisaa limoja baada ya kumtusua demu mmoja alie niletea dharau... Kama lock up pako vile!!!!! Jela je?
 
kuna tetesi kuwa msanii chidbenz amehukumiwa miaka miwili jela,mwenye taarifa kamili atujuze hapa
 

Attachments

  • 1424948649051.jpg
    38.1 KB · Views: 362
Kumbe ukikamatwa na ngada hauendi jela siku hizi?
 
chidi benz amefanikiwa kulipa faini ya laki 9 hapo hapo mahakamani na kuondoka akiwa huru kabisa
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leoimemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh.900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya. Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.


Chanzo: GPL
 
chidi benz amefanikiwa kulipa faini ya laki 9 hapo hapo mahakamani na kuondoka akiwa huru kabisa

madawa ya thamani ya shilingi million 38 na fine laki 9

hii ni ndio biashara ya kuwekeza
 
madawa ya thamani ya shilingi million 38 na fine laki 9

hii ni ndio biashara ya kuwekeza

mkuu ulisoma vibaya.Soma tena hapa chini.
Faini anayotakiwa kulipa ni shilingi laki tisa. Chidi alikutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 38,638, na bangi yenye thamani ya shilingi 1,720 pamoja na na vifaa ya kuvutia dawa hizo ambavyo ni kijiko na kigae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…