"CHIDUDU" Dawa kiboko ya maleria, haina mfano.

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Ni dawa ya asili ambayo ina karaha kidogo yaani yataka moyo,
huwezi kuamini ndani ya masaa machache unakuwa umeshapata
nafuu.

Inafanywa hivi,
Chemsha maji yawe ya moto kiasi ambacho mtu anaweza kuoga
bila shaka kwa wale wa maeneo ya baridi wanafahamu vema joto
la maji ya kuoga.

Chukua Keni ile inayotumika kuingizia mafuta ya kula au ya taa kwenye
chupa yenye mdomo mdogo, Ingiza hiyo Keni makalioni kisha miminia maji
hayo ya moto makalioni kupitia hiyo keni.

KITAKACHOTOKEA:
Utaharisha sana. Zoezi hilo litaisha kwa kujisikia hamu ya kula na
kujikuta ukirudiwa na afya. Najua wapo wanaoifahamu vizuri dawa
hii ya aina yake naomba wanisaidie kutoa ushuhuda wao hapa ili isije
kuonekana kuwa ni utani.

KILA LA HERI KWA WATAKAOJARIBU.
 

Kwanini utumie njia ya mkato, ukinywa hiyo dawa inakuweje, au ni "external use only, keep out of reach of children"
 
acha masihara kaka......hii dawa itumie tu mwenyewe
 
acha masihara kaka......hii dawa itumie tu mwenyewe

Kweli kaka hiyo dawa nimewah isikia Mtwara lakin niliambiwa ni ya kiuno sio malaria nadhan wamakonde wengi wanaifahamu!hizi dawa zingine unaweza kuwa aunt hivihivi
 
Hii inaitwa Hot water enema. Tumia distilled water -ndiyo nzuri zaidi. Pia, badala ya kutumia keni, kanunue enema bottle kwenye pharmacy
 
Kwanini utumie njia ya mkato, ukinywa hiyo dawa inakuweje, au ni "external use only, keep out of reach of children"
E bwana siyo dawa ya kunywa hiyo mtindo wake ni huohuo
baada ya hapo ni mwendo wa kuharisha tu mpaka unapona.
 
acha masihara kaka......hii dawa itumie tu mwenyewe
e bwana sio masihara, hilo la kutumia au kutotumia utajua mwenyewe
lakini ni dawa ambayo inatibu maleria kwa masaa tu, wengi wanaofanyiwa
hupona haraka sana.
 
Kweli kaka hiyo dawa nimewah isikia Mtwara lakin niliambiwa ni ya kiuno sio malaria nadhan wamakonde wengi wanaifahamu!hizi dawa zingine unaweza kuwa aunt hivihivi
Ni kweli mkuu ilikuwa inafanywa sana Mtwara miaka ya
nyuma na watu walikuwa wanapona bila kwenda hospitali
si ya kiuno, narudia tena si ya kiuno ni ya Malaria nasisitiza
inatibu haraka sana na huwezi kuwa Aunt. Sina uhakika
kama bado inaendelea kutumiwa.
 
Mkuu GAZETI hii dawa yako mpaka sasa ninaifikiria lakini inanichanganya kidogo unajuwa kiswahili kimenikimbia sipo Anyumbani miaka 20 iliyopita hii kitu inaitwa keni ndio nini? Au keni unayokusudia ule mrija wa kuingizamafuta wakati unapokwenda dukani kunuwa mafuta ya kupikia? na Hayo maji unajimiminia kwa kiasi gani cha kiwango cha hayo maji?
 
Last edited by a moderator:
nadhani anamaanisha FUNNEL kama ile ya kupimia kerosene dukani:becky:
 
Aaah kashafanywa huyu
Bibi yangu alikuwa anafanya sana hiyo kitu, tatizo lilipo ni kuwa
wengi waliokuwa wanafanyiwa ni watoto kwa sababu kwa mtu
mzima mara nyingi ilikuwa inafanyika usiku hivyo ni ngumu
kujuwa ni nani anafanyiwa lakini kwa mtoto ni rahisi.
 
Ndio naukusudia huo mrija mkuu, kwa nilivyooona hii dawa haina kiwango
maalum yaani ni mwendo wa kukadiria tu kama zilivyo dawa nyingi za asili
nilichogundua hapa lililo muhimu ni kule kuharisha, sasa sijafahamu vijidudu
vya maleria hupotea vipi kwa kuharisha?
 
Mkuu GAZETI ningelikuwa huko Afrika ningeliwafanyia wagonjwa wa Malaria lakini nipo huku hakuna Mdudu anayeitwa Mbu kuna baridi kali hata huyo Mbu akiwepo atakufa kwa baridi asante sana.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…