Kwa mujibu wa Sheria yetu ya ndoa ya Mwaka 1971. Kama watoto wana umri wa chini ya miaka 7. Watoto watatunzwa na mama ambapo baba atawajibika kutoa matunzo na visitation right.
Kama wana umri wa zaidi ya miaka saba, wazazi mkubaliane wakae wapi. Msipokubaliana, yaani mkiamua kuwagombea, mahakama itaangalia the best interest ya watoto ikiwepo kuwauliza watoto wenyewe.
Mmoja ya wazazi akiweka pingamizi la kipato/ulevi au ukatili dhidi ya watoto, mahakama inaweza kuamua kumkabidhi mzazi salama na baba kuwajibika kutoa matunzo.
Sheria yetu hii inatamka bayana kiwango cha matunzo ni Shilingi Mia moja kwa kila mtoto kwa Mwezi!.
Pia ni sheria ya mfumo dume kuwa baba tuu ndio mwenye jukumu la kutoa matunzo hata kama baba ni jobless na mama ndio mwenye kipato.
Wanaharakati wa haki za binaadamu/jinsia/watoto wamepiga kelele sana kuhusu sheria hii kupitwa na wakati mpaka sasa hakuna kilichobadilishwa japo ustawi wa jamii na mahakama vimekuwa vikitoa maamuzi kuongeza kiwango cha matunzo from time to time.