Chill Boys yaachana na aliyekuwa kocha wa Yanga Luc Eymael

Bon-CN

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2020
Posts
1,514
Reaction score
3,000
Yule kocha mtukutu na msema hovyo ambae aliwahi kuwata Watani kwamba Manyani, kauli yake hiyo inaendelea kumtafuna. Baada ya Eymael kutupiwa virago na Vyura wa Bwawa la Jangwani, miezi michache baadae, Chippa United, maarufu kama Chilli Boys wakaonesha nia thabiti ya kumpa mkataba.

Kama tujuavyo undugu tuliona nao kati ya Nyumba ya Julius Kambarage, na Home kwa Babu Mzee Madiba, chama cha soka nchini humo kilianza kupinga mwanzoni kabisa wakati Chilli Boys walipoonesha nia ya kumpa ajira Kaburu huyo kutoka Ubelgiji.

Nadhani Uongozi wa Chilli Boys wakadhani SAFA wanatania kutomtaka Kiboko ya Watani lakini baada ya kukumbana na pressure kutoka kila kona hususani kutoka SAFA pamoja na Serikali ya Jimbo la Eastern Cape, hatimae Chilli Boys wameufyata mkia.

Sehemu ya taarifa ya Chilli Boys inasema:



Kwa kweli sifahamu niligusa nini lakini ghafla nikakuta thread imeniponyoka kabla sijaimalizia vizuri, matokeo yake hata heading niliyokuwa nimeandika mwanzo, baadhi ya maneno yamekatika. Kutokana na mapungufu hao, endapo itawapendeza basi badilisheni hiyo heading ili iendane na content.

Heading kama "Kauli ya Kibaguzi Wakati Akiwa Yanga, Yamfanya Luc Eymael Atumbuliwe Tena" nadhani itapendeza zaidi.
 
Yule kocha anashambuliwa bure kila siku kauli yake inaonyesha alikuwa mkweli
Mimi mwenyewe ni Mnyama lakin cwez kuunga mkono kauli ya kibaguzi kama zile. Hivi kama mashabiki wa Vyura wanabweka kama mbwa na tumbili, Shabiki wa Mnyama wana tofaut gani na wale wa Vyura? Kuunga mkono kauli kama hizo ni sawa na kuunga mkono kwamba hata mashabiki wa Mnyama nao ni kama tumbili na mbwa kwa sababu hatuna tofauti yoyote. Hapa tuombee platnam tuwatoke vinginevyo tutakuja kuambiana hapa tuna tofauti gani. Na kwa kifupi, mashabiki wote wa soka duniani ndo wapo hivyo

Yote kwa yote, waliompiga chini hivi sasa ni wale wanaojali heshima na utu wa mwafrika, kwahiyo wewe baki na u-Simba wako over your race lakini mbele ya akina Luc, sote sisi ni matumbili tu
 
Weww ni utopolo unayejificha kupitia mnyama
 
Kama kupinga ujinga na utopolo basi hata Haji Manara na mwenyewe ni utopolo. Endelea na kutojielewa kwako lakini wanaojielewa, washampiga chini, kamtetee kwamba alikuwa sahihi. Na-log off
Maswala ya Haji Manara hayanihusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…