Chimbo la used spares za magari Dubai

HSIRAJI

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2019
Posts
745
Reaction score
1,550
Wakuu habarini za jioni

Msaada wakubwa mwenye kujua ama Idea wapi kwa Dubai naweza pata used spare kwa magari tofauti kwa ajili ya kuleta bongo. Na siyo mbaya ukashare experience pamoja budget ambayo unaona ni sahihi kwa kuanza nayo.

Na vipi gharama za usafirishaji kwa contena pamoja na gharama za TRA bandarini?

Please, share any experience. Kwa ajili ya kujifunza na kupata fursa zaid kwa wengi.


Master of the game
Mshana Jr
JituMirabaMinne
GENTAMYCINE
Bujibuji Simba Nyanaume
 
Sina uzoefu sana wa Dubai, nimeenda mara chache na sikua nashughulika na spea. Nafikiri kama kuna sehemu ya kupata vitu vingi used vya magari basi nenda Sharja. Huu ni mji mdogo uliopo nje kidogo ya Dubai tuliyoizoea. Ni mwendo wa kwenda na kurudi siku hiyo hiyo, sio mbali.
Huko naona hata vijana wengi wa kipemba wanaenda kununua vipande vya mgari na rim used na vifaa vingine. Kwa Dubai kama lipo soko basi litakua sio kubwa
 
Shukran mkuu KWA msaada wako
 

Jaribu kuwacheck KilimanjaroStarCargo...hawa ni wasafirisha mizigo, kampuni pacha ya wale SilentOcean ndugu moja na kina GSM wa Yanga...

Kuna wakati walikuwa wanatoa muongozo wa soko la spare ambalo lipo Al Ayoun
 
Nashauri achana na Dubai pata Japan direct
 
Mimi niko Japan kazi ya kukata magari na kusafirisha nchi mbalimbali nimeifanya kwa muda mrefu ila kwasasa tumebadili nfumo wa kusafisha, tunauza online kabla ya kusafirisha mizigo ,

Ushauri wangu kabla ya kwenda Dubai fanya utafiti aina gani ya spare unataka kuuza, magari makubwa au madago Engine na giabox au vifaa vya umeme kama taa, control box ,starter , au vifaa vya body milango vioo ,kwakifu kuna aina nyingi za spare parts

kama unaplan kufanya biashara za Engine na giabox nakushauri usinunue Dubai bora ununue Japan kupitia kwenye page yetu Urgently Wanted in Japan unaweza kuandika list ya magari unayotaka kwajili ya spare kisha toa maelekezo jinsi ya kuyakata utapewa bei jumla pamoja na ushuru.

Uikipita ilala kwenye spare za used kutoka Dubai ukaongea na wafanya biashara wazoefu kunachanga moto nyingi sana ukinunua Engine 10 unaweza kufika Dar ukakuta zote mbovu tofauti na Japan tunakata magari yanayotembea .
 
Mtaji wako ni bei gani?
 
Mbona link yenyewe haifunguki mr
 
Mkuu watu wanakuuliza mtaji wako ni kiasi gani ili wakupe ushauri hausemi.
Haya mimi niko Dubai nipe kazi nikufanyie,hakuna sababu ya wewe kuchoma nauli kuja Dubai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…