Elections 2010 Chimbuko la Dowans/Richmond na uchaguzi wa Igunga

Elections 2010 Chimbuko la Dowans/Richmond na uchaguzi wa Igunga

beko

Senior Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
189
Reaction score
91
Hukumu ya Dowans imetoka wakati Muafaka ambao kampeni za mwisho zinafanyika igunga, Wapiga kura wa igunga tambueni kuwa ubovu na ufisadi wa CCM na Rostam Azizi ndio uliopelekea taifa hili lilazimike kulipa mabilioni haya, Tarehe 2 October iwe siku ya kuwapa Chadema ushindi ili kuowaongezea nguvu bungeni waweze kupambana na udhalimu huu na hatimae iwe ndio ishara ya kuwaondoa magamba 2015. Watanzania tunahitaji mabadiliko, tumenyonywa vya kutosha na tusipoamua sasa tutaangamiza taifa hili. Umaskini unazidi, maisha yanazidi kuwa magumu, hakuna anaejali hatma ya umaskini huu, wenzetu wametumia nguvu ya umma kuleta mabadiliko na kuondoa utawala dhalimu duniani, tanzania kwa nini tusifanye hivyo?
nawakilisha

Soma
 
Malipo ya Dowans kufanyika kipindi hiki ni kwamba watu wengi hamuelewi. Hii ilikuwa katika makubaliano kati ya CCM na Rostam ili aweze kuwasaidia Igunga, moja ya sharti ni kwamba serikali lazima iisaidie Dowans kupata malipo yake haraka iwezekanavyo kabla ya Uchaguzi kufanyika.

Watanzania tumekwisha!
 
watatumaliza yaani nikona mtu kavaa kofia na vile vitishet vya ccm natamani nimtie ngumi coz ni mjinga
 
Mbona hamsemi kuwa Dowans sasa ni Symbion? Kinawazuia nini?
 
hUkumu hii imejibu swali langu kuhusu nini Rostam aliahidiwa kurudi igunga kula matapishi yake?
Jibu
Kesi yako ya bill 92 itahukumiwa kabla ya uchaguzi Igunga.
Jicho la Mungu linaona,watanzania wanaona na dunia inaona, malipo ya mafisadi yapo hapa hapa Duniani, Mubarak Example
 
Huu ni wakati muafaka kwa wana IGUNGA,
Malipo yaDowans(Rostam Aziz,Kupanda kwa Mafuta,kukosekana sukari..............................
 
Japo sina taarifa sahihi juu ya ahadi ya RA lakini katika mtizamo tu wa kawaida hili ni jibu la RA kurudi kula matapishi yake hata kabla ya waliozimia wakimlilia hajawa discharged from hospital.na inataka ujasiri wa ajabu,tena inahitaji roho ngumu sana,ukusanye watu uwatangazie unaachana na siasa uchwara zilizokuchosha halafu baada ya muda mfupi unajitokeza tena kwa umma huo huo na kupiga kampeni za mtu anaegombea kupita chama chenye siasa uchwara zilizo kuchosha na ukaamua kuachana nazo,hili linahitaji roho ngumu sana,na kwa kuwa pesa ni shetani nadhani huyu RA alikuwa amepewa ahadi maalumu na kweli yametimia.
Igunga tunawategemea sana kuleta mabadilioko kwani sanaa iyote imefanyika mbele zenu leo itakuwa ni ajabu kubwa kama mtu utajilawa asubuhi kwenda kumpigia Dalaly wa madini anaegombea kupitia chama chenye siasa uchwara.siamini kama mtakuwa vipofu kiasi hicho,fanyeni maamuzi sahihi,huu si wakati wa kugeuzwa watoto.
Kila la heri Igunga
 
Nikiifikiria sisiemu kichwa kinaniuma.
 
Nnatamani sn kama huku Tz kijana akibalehe nae aruhusiwe kumiliki AK47 kama wafanyavyo Waarabu,nnadhani hapo tungeheshimiana sn sababu mdomo pekee haufanyi kazi kwa viongozi wetu ni Kama wameweka pamba masikioni.
 
Wana-Igunga, huo ugumu wa maisha mnaouona ni kwa mtaji wa ufisadi wa Mhajemi Rostam Aziz na uporaji kupitia Dowans. Na kwa kuwa CCM ndio hivo wamekubali kulipa UFISADI kwa hiyo kampuni hewa, ndio kama hivo tutarajie gharama ya maisha kupanda zaidi.
 
Yaani haya mambo yanaumiza kichwa ukiwaza sana juu ya tz unaweza kuugua kichaa, kikubwa watu wa igunga wasituangushe mifano hai wanayo. CCM inatumaliza jamani watz tuamke.
 
Back
Top Bottom