Chimbuko la wapogoro

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Wapogoro ni kabila la watu kutoka kusini-kati ya nchi ya Tanzania, hususan mkoa wa Morogoro.
Lugha yao ni Kipogoro .

HISTORIA

Inasemekana asili yao ni Afrika Magharibi, hasa katika nchi ya Senegal, pia Afrika ya Kati Congo. Kuna mila nyingi Senegal na ngoma zake nyingi zinafanana na Sangula. Sababu ya kuhamia Tanzania ilikuwa utafutaji wa ardhi ya kilimo na mabadiliko ya hali ya hewa . Waliendelea kuhama zaidi kutoka Senegal na wengine walikimbilia pia Zambia, Zimbabwe na Malawi. Ndiyo maana kuna ukoo mkubwa wa Matimba kule Malawi na huko Zimbabwe.
 
Na kabla ya kufika senegal walitokea wapi?

Si bure kule senegal nao wanasema wapogoro asili yao ni Afrika Mashariki huku.
 
Wapogoro wana Sifa jamani..
Wanapenda shuguli mno
 
Kwa hiyo... Hao wahamiaji kutoka Senegal walipofika MAHENGE "KULIBOMA" Hawakukuta wenyeji?
 
Historia bana...eti wapogoro wana asili ya kina Mane. Aisee
 
Naamini mkuu. Kama naamini sisi wanadamu tumetokana na sokwe. Nitashindwa kweli kuamini kitu kidogo hivyo kuwa Wapogoro wanaundugu na Wolof?
Makabila mengi hapa Bongo ni wahamiaji.
Hivi nikikwambia Wangoni wana undugu na akina Lucky Dube au Mariam Makeba utakataa?
 
Acha uwongo jinsi wapogoro walivyowavivu watatafutaje ardhi ya kulina!!! Eti sababu ya kuhamia Tanganyika ni kilimo! Hao ni ndwanga milimo kama mbunge wao Mlinga
 
Na kabla ya kufika senegal walitokea wapi?

Si bure kule senegal nao wanasema wapogoro asili yao ni Afrika Mashariki huku.
Akikujibu hapa ni-tag kwa sababu!!
Senegal kule jamani sijui Cameroon! ni mbali kwa nyakati zile za hatari, Hapo Msitu wa Congo, Umanyema walivukaje? kwenye utwala wenye makeke??? si ke'' wangeolewa wote? vidume msoto kuuzwa, vinginevyo wapite porini waliwe na simba!! Halafu hapa EA Mfalme wa Ethiopia ndiyo alikuwa mbabe wetu akiingia mgeni tu ke anaolewa me'' anafanywa mtumwa faster!

Zamani falme ikisafiri uwe na jeshi mahiri, lenye TISS wenye mbio na mbinu za kichawi hasa, halafu na hela ya kulipa ushuru, zaidi ya hapo ni majanga tu! kulikuwa na kiongozi mwenye Makarama km Shaka zulu???! akisikika anapita na watu wake aliandaliwa zawadi za Ng'ombe kabisaaa!!! na mabinti vigori!!! ili kumtuliza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…