China Imefungua hospitali ya kwanza yenye kutumia Maroboti

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
China Imefungua hospitali ya kwanza yenye kutumia Maroboti

Teknolojia ya Akili mnemba (AI) Inazidi kushika kasi ulimwenguni, sasa teknolojia hii imepelekwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya.

Nchi ya china ikishilikiana na chuo cha Tsinghua university imefanikiwa kufungua hospital yenye kutumia teknolojia ya Ai ikiwa na madaktari 14 wa Ai wenye kukufanyia uchunguzi na kukupatia matibabu kwa ufasaha.

Wale wagonjwa wote wa kibinadamu wanakua wanapatiwa matibabu na madaktari wa AI, hospital hiyo inaitwa Agent Hospital. Kuanzia wauguzi , manesi na madaktari wanakua wanaendeshwa na muundo wa LLM (large language Model) wenye Uwezo wa kuingiliana kwa urahisi.

Cha kushangaza zaidi ni Uwezo wa madaktari hao wa kiroboti kuweza kuhudumia wagonjwa wengi kwa wakati mmoja yani ndani ya siku chache Wanaweza kuhudumia wagonjwa 10,000.

Kwa upande wa madaktari wa kibinadamu ingechukua miaka miwili kuweza kuhudumia wagonjwa hao.

Wengi wanawaza Je teknolojia ya AI inaweza kuchukua nafasi ya binadamu?? 😮

#bongotech255
 
Nafanya ya kazi ya technical support kuhakikisha DaVinci robot inafanya kazi ipasavyo ambayo daktari anakaa kule huku akitumia joysticks na mgonjwa kule kwenye kitanda
Maana yake PS4 na XBOX zipewe maua yake....

Hivi lile la Nape lipo wapi Kwa sasa nchi inatakiwa ccm wote wafe aisee😥😥😥
 
Tunaweza kufurahia kwa sasa lakini hili lina athari kubwa sana kwa ustawi wa binadamu.. Kwakuwa kila kitu sasa kitafanywa na robot then mwisho wake binadamu atafanya nini?
 
Tunaweza kufurahia kwa sasa lakini hili lina athari kubwa sana kwa ustawi wa binadamu.. Kwakuwa kila kitu sasa kitafanywa na robot then mwisho wake binadamu atafanya nini?
Binadamu anapaswa kula Bata tu mkuu, kazi zote zifanywe na machine
 
Tunaweza kufurahia kwa sasa lakini hili lina athari kubwa sana kwa ustawi wa binadamu.. Kwakuwa kila kitu sasa kitafanywa na robot then mwisho wake binadamu atafanya nini?
Binadam hawezi kukosa cha kufanya.
Atatengeneza robot
 
Sipati picha robot anapopima njia ya uzazi ya mwanamke mjamzito...

Pigishwa katerero...

Cc: Mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…