China imeunda Roboti zinazoweza kupigana

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240

Kampuni ya Unitree ya kuunda Roboti aina mbalimbali imeonyesha Roboti mpya aina ya G1 Humanoid yenye uwezo wa kupigana kwa kufundishwa ndani ya dakika 3 na kuweza kufanya Kila kitu kwa usahihi.


Kwenye video moja iliyopostiwa mtandaoni sio ya kutengenezwa ni uhalisia ikionyesha Roboti akiwa na uwezo wa kupiga mapigo ya Kung Fu bila kusahau uwezo wa kuruka mateke ya kuzunguka nk.


Roboti huyo anauzwa kwa Dola $16,000 ikiwa na injini 23 mpaka 43 zinazomuwezesha kutembea, kukimbia, kurukaruka, kupiga ngumi na hata kucheza. Roboti awa tofauti na wale wa Magharibi kama vile Tesla na optimus Yenyewe G1 Ina uwezo wa kujilinda inapoona hatari mbele yake.

angalia video yake ✍️.....!!!!! 👇

Your browser is not able to display this video.
 
"Binadamu wa sasa uwezo wao wa kufikiria kwenye ubunifu umepungua sana hiyi baada ya kuwaza pesa na umaarufu".
 
Kwa robot huyo akirusha teke mpaka azunguruke, nipeni kipande cha nondo kisha nile pilipili nyingi, namkalisha mapema sana.
kumbuka ni lichuma hilo ndugu...😅
 
Ziletwe huku zije kupigana na M23 na CCM.
 
Wamuozeshe yule roboti wa Elon wapigane mimba wasituchoshe…!!
 
Lile roboti la akina Nape liliishia wapi?
 
Liko slow sana kukatwa mitama kama yote
 
Wajitahidi kuongeza specification kwenye zile roboti pendwa za mizagamuano, hizi kwa hapa Tz hatuna shida nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…