Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Mkutano wa mwaka 2024 wa Kazi ya Uchumi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China unafanyika hapa Beijing. Mkutano huo utachambua hali ya sasa ya uchumi wa China, na kuamua mwelekeo wa sera za kiuchumi kwa mwaka 2025. Ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, China ina imani ya kudumisha ukuaji tulivu wa uchumi.
Tangu mwaka 2019, ingawa uchumi wa dunia umeendelea kudorora kutokana na changanmoto mbalimbali, zikiwemo COVID-19, vita na mivutano ya kibiashara, uchumi wa China umedumisha ukuaji mtulivu. Hasa wakati wa janga la kimataifa la COVID-19, China ilikuwa nchi kubwa ya kwanza kufufuka kwa uchumi, na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia.
Mwaka 2023, Pato la Taifa la China lilizidi dola trilioni 17.79 za Kimarekani, na ongezeko la pato hilo kwa mwaka 2023 ni sawa na pato la jumla la nchi yenye ukubwa wa kati. Shirika la Habri la Marekani Bloomberg linatarajia kuwa China itaendelea kuwa mchangiaji mkubwa zaidi wa ukuaji wa uchumi wa dunia katika miaka mitano ijayo.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, China imeendelea kudumisha ukuaji mtulivu wa uchumi, na katika robo tatu zilizopita, Pato la Taifa la China lilikua kwa asilimia 4.8. Tangu mwezi Septemba, kutokana na sera za kuchochea uchumi kuendelea kutekelezwa, uchumi wa China umedumisha mwelekeo wa kuimarika zaidi, na unatarajiwa kutimiza lengo la ukuaji wa asilimia 5.0.
Biashara ya nje, uwekezaji na matumizi ni nguzo tatu kuu za maendeleo ya uchumi wa China. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, katika miezi 11 iliyopita ya mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara ya bidhaa kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu dola trilioni 5.5 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 2.1. Aidha, hadi mwezi Oktoba, uwekezaji wa viwanda nchini China umeongezeka kwa asilimia 9.3.
Wakati huo huo, matumizi nchini China pia yanaongezeka kwa haraka. Kutokana na takwimu zilizotolewa na majukwaa ya biashara ya mtandaoni, wakati wa “Siku ya Manunuzi ya 11, Novemba”, mauzo ya aina 519 za vifaa vya nyumbani yaliongezeka kwa asilimia 200 ikilinganishwa na mwaka jana.
Hata hivyo uchumi wa China unakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo vita, hali tete ya kibiashara, kudidimia kwa uchumi wa dunia, na vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi. Lakini wakati huo huo, China ina uwezo mkubwa wa ndani, ikiwemo mfumo maalumu wa kijamaa, watu bilioni 1.4 wanaochapa kazi, soko kubwa la ndani, na mtandao kamilifu wa viwanda. Hivi vyote ni vyanzo vyenye nguvu vya ukuaji tulivu wa uchumi wa China.