China kujenga kituo kikubwa cha biashara Bagamoyo

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
2,364
Reaction score
867
Wasalaam wakuu!
Kama headline inavyojieleza hapo juu na hizo bahari ni za ukweli kabisa nanimafanikio ya safari ya Kinana na viongozi wengine wa ccm ndani ya Uchina.

Kaswahili kangu mie: Kwa nini bagamoyo na sio Dodoma ama Mwanza? Yale maneno ya mtaani kuwa kila rais ajae huandaa mazingira ya eneo lake kiuchumi yanaweza yakawa na ukweli wowote?
Na kwa nini Bagamoyo au dar tu isiwe Mwanza,dodoma ama mbeya?
Butiama kukoje mpaka sasa? Kwa mwinyi je? Mkapa kwao? Ana Rais ajeye kwao leo kukoje?
Kwa nini serikali yetu isiboreshe mazingira ya mikoa yote hasa inayokua Kiuchumi ili vijana wengi tusikimbilie dar es salaam?
 
Labda soko aidha la
PHP:
balakashia
au samaki changu...
Kiongozi hao watu wa balakashia wanakujaje kwenye mjadala huu kwani hawana haki nchi hii? ni bora uka angalia potentiality ya bagamoyo kwa mradi huu achani ubinafisi au unataka kikajengwe Moshi vijini
 
Kiongozi hao watu wa balakashia wanakujaje kwenye mjadala huu kwani hawana haki nchi hii? ni bora uka angalia potentiality ya bagamoyo kwa mradi huu achani ubinafisi au unataka kikajengwe Moshi vijini

Mkuu msamehe tu jamaa ni maoni yake ila thamani yetu sote ni moja
 
Ulitegemea nini baada ya kumwachia prince wake kila pande la ardhi,kila dini,kila mbuga,kila bonde na kila ziwa na mito watapewa wachina tuendelee kulala tutashangaa 2015 nchi imeuziwa wachina yote asilimia 99.8
 
Mh Kikwete ni mbunge mzuri sana wa Bagamoyo. Wabunge wote wanatakiwa kufanya kazi hivyo.
 
Acheni siasa bagamoyo ina pontential nzuri kwanza iko karibu na jiji kuu la uchumi dsm ambapo hata serikali imebase pia kule kuna mradi wa bandari ambao ni muhimu kwa kusafirisha na kuingiza bidhaa zinazohitajika pia suala la bandari nalo watu wanaleta siasa eneo la bandari dsm ni ekari 44 wakti mwambao wa bahari wa from bagamoyo to tanga na almost hekta elfu 23 sasa kuna maana gani ya kuendelea kung'ang'ania dar wakat kuna eneo liko wazi la maelfu jirani tu hapo bagamoyo na why mnakomalia bagamoyo tu mbona pia miradi ya bandari kavu,airports na vituo vya biashara inajengwa kigoma,mbeya hamuongei au JK huko kwao pia?ishu ni kua kigoma ni eneo strategic 4 business sasa mlitaka kijengwe wapi singida au
 

Hatupingi ila tunaunganisha dot tu
 

Unajua uwanja wa ndege wa mby ,umechukua zaidi ya miaka mingapi?unajua bandari ya Tanga ni muhimu kiasi gani na ina kina kiasi gani?Acheni mapenzi yaliyopitiliza.Potentiality ya mbeya kiuchumi na bagamoyo unaweza kuilinganisha?
 
Wacha ajenge ila ajue baada ya miaka 2 atajikuta jirani zake ni Wachagga na Wahaya na Wakwere hawapo. Sasa hivi wanauza ardhi wananunua pikipiki.
 
Binafsi sifurahii hii movie ya Bwagamoyo kuwa sehemu ya Dar ingawa si mkazi wa B/moyo,inatakiwa iwe set-lite town ya Dar na si part ya Dar,hii ni kwa ajili ya kutunza mji mkongwe ambao UNESCO wameshauorodhesha kama biosphere reserve ni fahari kuwa na mji wa zamani mzuri na msafi wenye utamaduni wake wa asli na kumbukumbu ya biashara za utumwa na nyara hapo kale huu ndiyo urithi wa asili siyo maghorofa makubwa na wachina wakirandaranda kila kona,hivi tutajivunia nini kizazi hiki kama tukiharibu kila jambo jema lililoachwa na viongozi wetu waliotangulia?.sioni kama hizi ni sifa mimi naziita za kijinga.
 
Unajua uwanja wa ndege wa mby ,umechukua zaidi ya miaka mingapi?unajua bandari ya Tanga ni muhimu kiasi gani na ina kina kiasi gani?Acheni mapenzi yaliyopitiliza.Potentiality ya mbeya kiuchumi na bagamoyo unaweza kuilinganisha?

Kwaiyo kama airport ya mbeya ilichelewa na bagamoyo isijengwe kisa airport ilichelewa au unamaanisha nini?mbona mkapa alianzisha ujenzi wa daraja kusini cha ajabu kipi au kuna maeneo fulani hayafai kujengewa fursa tatizo ni ukanda na chuki binafsi kwa JK mie pia siridhishwi na uongoz wake lakin mengine tunamuonea bomba la gesi linafahamika lilikua linaleta kwenye kituo kinyerezi watu oooh anataka kupeleka bagamoyo acheni siasa
 
Nadhani leo ni mara ya kwanza kukubaliana nawe. Nimekugongea senksi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…