MwanajamiiOne Naamini kila mtu hafurahii kwa uingizaji wa vitu vibaya na hasa vinavyoweza dhuru afya zetu.Lakini Solution unayopendekeza binafsi naona ni haiwezekani maana uki ban goods zote zinazotoka China maana yake ni kuwa humtakii mema Mtanzania wa kawaida, maana ukifanya hivyo utataka mwenzangu na mimi mwenye kipato cha chini anunue kiatu,simu,Computer,kijiko,kisu,nk kilichotengenezwa na Mmarekani au Ulaya kitu ambacho ni kigumu.
Kuna Wamerekani wenyewe wanaona vitu vinavyotengenezwa kwao wenyewe hawawezi mudu gharama za kununua na wanaishia kununua vilivyokuwa imported toka China,sasa sijui kwa sisi tunaoishi chini ya Dola moja kwa siku!!!
Njia sahihi ni kuboresha utaalamu tulionao katika kudhibiti bidhaa zinazoingizwa nchini kwetu, Kuondoa ufisadi uliokatika uingizaji wa vitu hivyo.
Pia the Best solution nafikiri kwa Tanzania yenye ardhi nzuri na hali ya hewa bora kabisa ukilinganisha na China haikutakiwa ingiza bidhaa za vyakula kama maziwa toka China!Ni aibu sana!!!!Tulitakiwa tuzalishe maziwa na kuwauzia wachina maana soko lao ni kubwa sana,Na wachina wenye akili kitu ambacho tumekizalisha in a more natural way Tanzania kwao wangetumia gharama yoyote kukinunua na kukitumia badala ya cha kwao hapa. Kuna vitu kadhaa ambavyo tunavyo Tanzania(including vyakula)wachina wanatumia gharama yoyote na wanavitumia kwao.
Tunatakiwa tufanye taratibu za kuhakikisha tuna import zile bidhaa nzuri tu kutoka China na Mbaya tuachane naz😵therwise China kwa sasa ndiyo producer wa asilimia kubwa ya vitu duniani na Nchi nyingi zimegomea mpaka sasa zimeshindwa na kukubaliana na hali halisi ya kuwa Mchina ndiyo huyo anainuka kutoka level aliyokuwa (pamoja na akina Tanzania) mpaka level ya juu.
Na nchi nyingine zinajitahidi tu kuhakikisha wanachopatiwa na wachina ni Quality goods na hili ndilo tunaloshindwa sisi. Na wachina wanachofurahisha ni kuwa ikithibitishwa kuwa mtu kaleta upuuzi kama huo wa kupeleka sumu nje ya nchi yao, haijalishi ni Waziri au nani anaadhibiwa vikali na nafikiri unajua adhabu yao ni nini.
Labda mwenzangu na mimi hauishi Bongo, Lakini mimi nikiangalia kila kitu nimetoa China toka kuvaa, vyombo vya ndani, simu, radio, viti vya kisasa, vifaa vya umeme, nyumba yangu vitu kibao ni vya China, Sasa sijui kama vingekuwa banned sijui na ka'uwezo kangu haka ningepata wapi hivi vitu!
Kaka ukipata muda nenda utembee China na ndiyo utagundua tatizo ni sisi utaratibu wetu wa kupata vitu toka kwa hawa jamaa ndo mbovu,jamaa wana kila kitu (kizuri na kibaya, cheap na Expensive, feki na original), Unachagua mwenyewe kutokana na Interest zako.
Na kila siku wachina wanapaa kwenda juu wanabadilika toka kutoa Feki mpaka Original, Sisi tunalala na kupiga kelele kwamba jamaa wanatuletea feki wakati hata maziwa tu yametushinda tengeneza!!!!!!!