China: Tiba asili zinavyochangia huduma za afya kwa jamii

China: Tiba asili zinavyochangia huduma za afya kwa jamii

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1665643557161.png


Ukizungumzia tiba asili kwa watu wengi picha inayokuja haraka ni kwa watu waishio vijijini au jamii ambazo hazijapiga hatua katika masuala ya matibabu, lakini ukweli ni kwamba imani hii sio sahihi.

Nchini China tiba asili ina mchango mkubwa katika ustawishaji wa afya sawa na ilivyo au ilivyokuwa katika mataifa mengi siku za nyuma.

Jambo zuri ni kwamba China imefanikiwa kuoanisha tiba asili na matibabu ya kisasa, na hivyo kupata matokeo muhimu katika utoaji wa huduma za afya kwa umma

Tiba asili nchini China ni kitu rasmi, kuna shule kwa ajili ya watalaamu wa tiba asili na karibu katika kila mji kuna hospitali ya tiba asili.

Madaktari katika hospitali hizo hutumia utaalamu wao kujua tatizo la magonjwa kwa kumuona mgonjwa, kushika baadhi ya viungo, harufu na sauti, lakini inapobidi hutumia vifaa vya kisasa ili kujua tatizo. Baada ya hapo mgonjwa huandikiwa dawa za asili ambazo huzitumia kwa kunywa au kula kulingana na maelekezo na hupata matokeo chanya.

1665643607705.png


Daktari katika hospitali ya tiba asili ya Guang'anmen iliyopo jijini Beijing Dk Cui Yonggiang alisema mamia ya watu hupata huduma katika hospitali hiyo kila siku huku akisisitiza kuwa mchango wa tiba asili katika huduma za afya nchini china ni mkubwa sana.

Yongqiang ambaye anasimamia idara ya ushirikiano wa kimataifa katika hospitali hiy,o alisema "Tuna ushirikiano wa karibu na mataifa mengine kwa mfano Afrika tunashirikiana na Tanzania kupitia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, tunatarajia kuongeza ushirikiano zaidi na mataifa mengine"
 
Back
Top Bottom