Nimecheka kicheko cha ubwege, ujinga na majilaumu.
Kiingereza wanasema, "the burning issue". Huku "site" tunasema "kinachobamba" kwa sasa ni janga la ubanwaji wa kifua na mafua al-maarufu Corona.
Tayari watu milioni 2.1 wamekufa na milioni 100 wameambukizwa. Wanasayansi wanahangaika kusaka chanjo na tiba. Sasa ukisafiri nje ya nchi lazima upimwe covido.
China (ilikoanzia ugonjwa) imegundua njia mpya ya kupima ugonjwa huu kwa haraka na hakika kuliko upimaji wa sasa wa kusokomeza kijiti pamba puani ili kupata makamasi ya ndani kabisa yaliyo na virusi.
Wataalamu hao wamegundua kuwa njia ya haja kubwa ni rahisi zaidi kupima corona. Kwa mujibu wa tangazo kupitia BBC jana jioni, ni kwamba kijiti pamba ikisokomezwa "huko" yapata nchi tatu (urefu wa kidole cha shahada) unaweza kuja na virusi vya CORONA.
Hii maana yake ni kwamba kila binadamu atakayepimwa corona atalazimika kumpa mgongo daktari akibong'oa ili kumpa wepesi daktari kuingiza kijitipamba "kunako" ili kuwasaka virusi kwenye kamasi zilizoko kwenye kuta za "huko".
Nashauri: Jikague usafi ila kama una fangasi basi utibu mapema usijekumpa kazi ya ziada daktari kukushauri. Lakini pia Nina mashaka, kwa "ubong'oaji" huu dunia nzima hatutoibua ugonjwa mwingine wa ajabu?
Yani unaenda na familia yako hospitalini kila mwanafamilia anajua "tumepimwa". Ama kweli shetani kazini.
Sasa ndo Magu analipata hili, sio tu hamtochanjwa bali hata vipimo vya ugonjwa huu utakoma. OVA!