Chinese fried beef

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Nyama 1 LB (isiyo na mifupa katakata vipande vidogo vidogo).

Thomu na Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai

Sosi ya Soya (soy sauce) 2 vijiko vya supu

Chumvi kiasi

Karoti 1

Maharage ya kijani (spring beans) 1 kikombe

Pilipili mboga kijani 1

Kabeji 2 vikombe

Vitunguu vya kijani 2 miche

Mafuta ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1) Katakata nyama vipande virefu vidogo vidogo.

2) Roweka Nyama kwa chumvi, thomu na tangawizi, pilipili manga, sosi ya soya kwa muda kama saa.

3) Katakata karoti vipande virefu virefu vidogo kiasi.

4) Katakata pilipili mboga

5) Kata Kabeji nyembamba kiasi.

6) Weka mafuta katika karai kaanga nyama mpaka iwive.

(Karai nzuri kutumia ni ya kichina inayoitwa 'wok' lakini sio lazima)

7) Weka karoti na maharage ya kijani (spring beans) endelea kukaanga kwa dakika chache tu.

8) Usiwache mboga zikawiva sana.

9) Tia kabeji na pilipili mboga na ukaange kwa dakika 1
10)katia vitunguu vya kijani

Tayari kwa kuliwa..
 
Kama huna mda hawaweza kutengeneza hii simple ambayo ni beef na broccoli...

1)Chemsha nyama weka chumvi,thomu ,ndimu na tangawizi
2)Ikiwiva weka tomato paste na broccoli 3)koroga vichanganyike vizuri baada ya dakika tano epua...

Waweza kula na wali ama ugari..upendavyo wewe tu....
 
Yaasalam yasalaam... Broccolli hapo umemaliza !!
 
Unaweza ku share recipe yako ya chinise fried rice kama unayo tafadhali? Mashallah mapishi unayajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…